Naanza
Andiko hili kwa kutambua na kuhamasisha Tukio la kipekee katika anga ya
usalama mitandao ambalo limekua liki azimishwa kila mwaka katika mwezi
wa October ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya
usalama mitandao duniani kote. Kwa mwaka jana katika kuukaribisha mwezi
huu Nilipata kuandika katika andiko linalosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" na baadae kutoa tathmini ya mwezi katika andiko linalosomeka kwa "KUBOFYA HAPA".
Naimani Mwaka huu Tanzania ita uchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao. Tatizo kubwa kubwa ni kua njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.
Naimani Mwaka huu Tanzania ita uchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao. Tatizo kubwa kubwa ni kua njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.
Leo
nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa
kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za
wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla
wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao
kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.
Njia
hii si nyingine bali ni “Awareness
Program” Yaani elimu ya uelewa wa uhalufu mtandao na namna ya kujilinda.
Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbali mbali za
uhalifu mtandao, athari zake, njia ya kujilinda, Na Namna ya kulinda wenzake.
Kwa
kupata
elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua
wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana
na
uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya
uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake
baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao
na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na
uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili
linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam
wa usalama mitandao.
Kundi
la mwisho ambalo ni wahalifu wanaofanya uhalifu huu makusudi ingawa wanajua
wakifanyacho na hawana utayari wa kuepukana na uhalifu huu mtandao nalo
linapunguzwa nguvu kwani watumiaji mitandao wanakua na uelewa wa namna wahalifu
hawa wanavyo fanya uhalifu na njia sahihi za kujilinda hatimae kundi hilipia
linakosa watu wengi wanaoweza kuingia katika mtego wao wa uhalifu mtandao na
kupungukiwa kasi na nguvu ya usambazaji wa uhalifu huu.
Inaaminika
asilimia zaidi ya 37% ya wahalifu wa kundi hili la tatu wanapokosa watu
wanoweza kuingia mtegoni wanajikuta wanakata tama na kujishughulisha na mambo
mengine tofauti na uhalifu mtandao.
Kumekua
na wimbi kubwa la makampuni mengi mbali na kua na teknolojia nzuri ya kuzuia
uhalifu mtandao bado yameendelea kugubikwa na uhalifu mtandao kutokana na
kutowekea mkazo swala hili la kukuza uelewa wa maswala haya ya usalama
mitandao. Pia mataifa mengi yameendelea kujipanga kwa kua na vitengo kadhaa vya
udhibiti uhalifu pamoja na kua na sharia sahisi za kudhibiti uhalifu huku bado
wimbi kubwa la wahalifu mtandao bado likiendelea kua kubwa.
Tatizo
ni kukosekana na njia sahihi na namna madhubuti ya kuendea njia hii ya kukuza
uelewa wa maswala ya usalama mitandao ambapo kama nilivyo fafanua awali
ingeweza kabisa kupunguza kwa kiasi kukubwa swala hili la uhalifu mtandao.
Kumekua
na jitihada nyingi za kuhamasisha kuanzia ngazi ya mtu binafsi, Makapuni ,
Nchi, Bara na hatimae Dunia nzima kujenga tamaduni ya kukuza uelewa wa matumizi
salama ya mitandao ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu unaoendelea kukua
kwa kasi hivi sasa.
Swali
linaloulizwa ni kwamba pamoja na jitihada nyingi za wanausalama mtandao ambapo hadi sasa pamoja
na mambo mengine, tayari kuna mwezi wa Kumi ambao unafahamika kama mwezi maalum
wa maswala ya uelewa wa usalama mitandao yaani “OCTOBER – Cybersecurity
Awareness Month” na kupatikana kwa
tamthilia maalum ambazo zipo kukuza uelewa wa usalama mitandao.
Jibu
ni kwamba, Jitihada hizi zimebaki kwa wanausalama mitandao na wananchi
wakawaida bado imekua ni vigumu sana kufikiwa na kuelewa pamoja na kua miongoni
mwa jitihada hizi.
Wengi
bado wamebaki wakijua swala la ufahamu na uelewa wa maswala ya usalama mitandao
ni swala la wanausalama mitandao pekee huku wengine wakiamini pia wana TEHAMA
ndio pia wanausika.
Inasahaulika
kabisa swala la kubaki salama kimtandao ni swala linalo takiwa kuanzia katika
ngazi ya mtu binafsi sawa kabisa na swala la ulinzi wa uhalifu mwingine wowote.
Tumekua na utamaduni wa pamoja na mambo mengine, kufunga milango, kuwa na
walinzi katika nyumba zetu na kuweka taa za nje tukiamini zinauwezo wa kusaidia
upungufu wa uhalifu majumbani mwetu.
Cha
kushangaza zaidi, Jitihada hizi binafsi huzioni zikiamishiwa katika udhibiti wa
uhalifu huu wa mitandao ambapo vitu kama Antiviruses, Maneno ya siri na
mengineyo ni ya kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi.
Kuna
Kila namna ya kufahamu kua pale swala la uelewa wa maswala ya usalama mtandao
litakapoweza kufanyiwa kazi kwa kiwango kizuri basin i wazi kabisa linaweza
kusaidia kila mmoja kuelewa na kuhimili ipasavyo uhalifu huu mtandao katika
ngazi ya mtu binafsi, pamoja na kukuza utamaduni wa kila mmoja kujua anajukumu
ssi tu la kujilinda binafsi kimtandao bali na kulinda wengine ipasavyo kuhakiki
taifa, bara na hatimae dunia inabaki salama kimtandao.
Kwa
ufupi nimefafanua kwa kina faida zinazoweza kupatikana pale uelewa sahihi wa elimu
ya usalama mtandao itapatikana kwa jamii zetu na katika maofisi yetu (Makampuni)
Maelezo hayo yanawea kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” Wakati huo huo nilipozungumzia
mambo muhimu yanayo paswa kuenda sambamba na uwepo wa sharia mpya ya usalama
mitandao niliainisha kwa kina swala la uelewa sahihi wa maswala ya usalama
mitandao pamoja na ujuzi wa kufanyia kazi uchunguzi wa uhalifu mtandao na
ushirikiano
KWA HISANI YA YUSUPH KILEO
Post a Comment