Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari jana kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar .Zifuatazo ni dondoo muhimu ya mkutano huo:
1.Katika Magazeti Yenu Jana mlimnukuu M/kiti wa TUME akijibu tuhuma za
UKAWA juu ya mazingira ya wizi wa Kura
2.Jaji Lubuva Jana amejibu kwa wepesi tuhuma za wizi wa kura
3. Lubuva anasema ukishapiga kura rudi Nyumbani. Nawaomba vijana na wapiga
kura wengine waipuuze kauli ya Jaji Lubuva!
4.Jaji Lubuva amedai yupo tayari kuziba mianya ya wizi wa kura. Nitataja mianya hiyo ili Jaji Lubuva ajibu
masuala haya!Mnyika: Matokeo ya Rais kubandikwa kituoni sio jambo jipya. Ni suala la
kisheria. Nawaomba watu wasome sheria ya Uchaguzi
5.Masanduku ya kura kupelekwa kituo cha majumuisho sio jambo Jipya.
6.Lubuva anasema matokeo yatascaniwa jimboni.Hili sio jambo jipya. Mwaka
2010 matokeo yaliyoscaniwa yalikuwa tofauti na karatasi halisi
7.Jaji Lubuva aseme hadharani, ni lini wataalamu wetu wa IT wakakague na
kuhakiki mfumo wa kutuma matokeo ili kuepuka goli la mkono
8. mfumo wa kujumlisha kura mwaka 2010 ulikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea uchakachuaji wa kura!
9.Jaji Lubuva amesema uhakiki umefungwa, kuna jambo kubwa limejificha.Kama hakuna uhakiki daftari limeshakuwa la kudumu!
10. Mpaka tunavyozungumza hatujakabidhiwa daftari la kudumu la wapiga kura, Takwimu zinazotolewa idadi ya wapiga kura haziaminiki!
11. Tume iseme ni kwa nini mpaka sasa hawajatoa nakala za "soft copies" kwa vyama vya siasa ili wazihakiki?Hapa bao la mkono limejificha
12. UKAWA na vyama vingine Lazima viende kuhakiki Database ya Tume Makao makuu. Kwanini Lubuva hataki sisi tuende kuhakiki?
13.Jaji Lubuva anasema ipo kamati ya IT, muulizeni hiyo kamati ya IT ya vyama vya siasa inaundwa na nani?
14.Majeshi kuandikisha namba za askari, IGP alikiri jeshi kufanya hivyo kwa baadhi ya mikoa, kuna kitu kimejificha!
15.IGP alikiri suala hili limefanyika, msemaji wa TPDF alikanusha, kauli zao zilikinzana.Tume iseme ni kwanini majeshi yaliandika namba?
16. Suala la kuhamisha watumishi wa Tume, limeamia kwa wakurugenzi baada ya Rais, kuteua mkurugenzi Mpya!
17. David Radio5: Wapiga kura wa Mara ya kwanza, na wasiojua utaratibu je wanabakia wapi baada ya kupiga kura?
18.Wapiga kura, wawe makini kuhakikisha wanapiga kura Siku ya tarehe 25 Oktoba!
19. Daftari la kudumu halitolewi kwa wakati ili kuruhusu goli la mkono!
20.Wapiga kura wajielekeze kuangalia majina ndani ya daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo!
21. Orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo inaandaliwa na manispaa, na daftari analopewa wakala limeandaliwa na Tume
22. Tume itoe Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva amesema atalitoa daftari Siku 4 kabla ya Uchaguzi, hapa amejichanganya!
23.Hatua ya pili ni kutoa 'permanent voter register' hili ilipaswa kutolewa mapema
24. Kuna madaftari mawili, provisional voter register, hili tulitakiwa kupewa kabla ya uhakiki wa wapiga kura, hili hatujapewa! 25. Rai yangu kwa wana UKAWA, wasikate tamaa kufuatia matamko ya mawaziri mbalimbali
26.Juu ya matumizi ya vyombo vya Serikali kujihusishanaUchaguzi, linaongozwa naraisi,Bunge limevunjwa ila baraza la mawaziri linaendelea
27. Iundwe kamati ya pamoja ya vyama vya siasa ya IT ikakague Daftari na kuliboresha ili kuzuia goli la mkono!
Swali la1: Tulianza kusema haya mambo mapema, waliamua kufumba masikio na macho!
Maswali:Fred kutoka Mtanzania: Kisheria mnatakiwa mpate soft copy ya Daftari baada ya Muda gani?
Maswali: Francis kutoka KTN: suala la uhakiki wa BVR hamuoni Siku zimebaki chache na kwanini msingeliibua suala hili mapema?
Mnyika: Tume iliwahi kukiri kuwa haiko huru mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, WaTZ wasikubali faster faster hii.
Mnyika: Wanapeleka huu mchakato faster faster, rai yangu tusisubiri tarehe 25 Oktoba, tuanze sasa kudhibiti goli la mkono!
Mnyika: Ndani ya nchi tunao watazamaji wasisubiri mpaka Uchaguzi uishe, waende Tume kutazama mfumo huu wa ujumlishaji wa kura
Mnyika: Nawaomba 'Waangalizi wa Uchaguzi' watoe ripoti zao mapema juu ya haya masuala!
Mnyika: Tume ya Uchaguzi sio Mali ya watu binafsi, ni tume ya Taifa letu.
Mnyika: Kijana ukishaona matokeo yamebandikwa, piga picha matokeo hayo na uyatume kwenye WhatsApp!
Mnyika: Kama kuna MTU ataniita mchochezi kwa kusema 'first time voters' wakae mita 200 kusubiria matokeo basi atangulie mahakamani,
Mnyika: First time voters, kukaa ndani ni kosa kisheria, kukaa nje si kosa kisheria, kisheria wanakaa mita 200!
Maswali: David Radio5: UKAWA mtafanya nini endapo tume haitafanya mnayosisitiza wafanye?
Mnyika: Nasisitiza BVR ni Bomu la kufungwa bao la mkono, yote tuliyosema yazingatiwe na wahusika!
Maswali: Prosper - The Guardian: Mnataka wataalamu wa IT wakakague daftari pekee, vipi kuhusu ukaguzi wa idadi ya kura zilizopigwa?
Mnyika: Kama Tume haitasikiliza haya tunayosema wanajitengenezea mazingira ya kupelekwa ICC!
Mnyika: Local monitors wa Uchaguzi wapo wachache, wanasubiria matokeo majimboni, kila mpiga kura lazim awe monitor!
Mnyika: Nje ya kituo cha kupiga kura sisi wapenda Amani, tutawalinda mawakala wetu, wasirubiniwe kupokea hongo ndani ya vituo vya Uchaguzi!
Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.
Post a Comment