|
Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia
Mahujaji
wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali
ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe
24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji
waliofariki dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya
mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo kufikia
ishirini (20). Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi
vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim
(Khidmat Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus
Anatory Rutayulungwa (Khidmat Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu
Daawa).
Wengine
ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat
Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu
Daawa).
Serikali
ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za mahujaji waliofariki
dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu
wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2015
|
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
MAHUJAJI
on Tuesday, October 13, 2015
Post a Comment