Tume ya Taiafa ya Uchaguzi (Nec). |
Vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimekubali
kusimamisha mgombea zaidi ya mmoja kwa ngazi ya udiwani na ubunge katika
uchaguzi mkuu ujao ili wananchi wenyewe waamue kupitia masanduku ya
kura nani wanayemtaka.
Awali, vyama hivyo vilikubaliana kusimamisha mgombea mmoja kwa kila
ngazi kuanzia udiwani, ubunge na urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba
25, mwaka huu.
Hata hivyo, kwa nafasi ya urais, vyama hivyo vinne vya NLD, Cuf, Chadema
na NCCR-Mageuzi, vimekubaliana kumsimamisha Edward Lowassa.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka vyama hivyo ambazo zilithibitishwa
na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, vyama hivyo kwa sasa
vimekubaliana maeneo ambayo kuna mgombea zaidi ya mmoja ambaye chama
chake kipo chini ya Ukawa, wote waendelee kugombea na wananchi ndiyo
watakaomua.
Vyama hivyo vilitangaza mgawanyo wa majimbo kabla ya kuanza kampeni za
uchaguzi, lakini majimbo 12 hayakupatiwa ufumbuzi wa namna ya
kusimamisha wagombea walio chini ya Ukawa.
Kwa mujibu wa Makene, kwa sasa Ukawa haina namna yoyote ya kufanya ili
kuweka mambo sawa kwa kuweka mgombea mmoja katika majimbo hayo pamoja na
baadhi ya kata ambako kuna zaidi ya mtu mmoja.
Alisema kwa sasa Tume ya Taiafa ya Uchaguzi (Nec), imeishachapisha
majina ya wagombea wote katika karatasi za kupigia kura na kwamba hata
kama Ukawa watamuondoa mgombea ili kumpisha mwenzake, bado jina lake
litaonekana siku ya kupiga kura.
Alifafanua kwamba kwa sasa kumuondoa mgombea kuna hatua ndefu kwani
atatakiwa kwenda mahakamani kuapa na kwamba Ukawa imeamua kata na jimbo
ambalo kuna mgombea zaidi ya mmoja wabakie hivyo hivyo.
Post a Comment