Tingatinga likishusha ukuta.
Likizidi kubomoaVifusi baada ya kubomoa. Wakazi wakitoa vitu vyao nje ya myumba wakati wa bomoabomoa. Wananchi wakitaharuki huku Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi na amani eneo la tukio.
Namna ambavyo ukuta ulivyobomolewa.
Likizidi kubomoaVifusi baada ya kubomoa. Wakazi wakitoa vitu vyao nje ya myumba wakati wa bomoabomoa. Wananchi wakitaharuki huku Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi na amani eneo la tukio.
Namna ambavyo ukuta ulivyobomolewa.
MANISPAA ya Kinondoni,
jijini Dar es Salaam ikishirikiana na Wizara ya Ardhi inaendelea na
oparesheni maalum ya kubomoa nyumba zilizojengwa kinyume na sheria
katika manispaa yake, oparesheni hiyo leo imetinga maeneo ya Mbezi Beach
na kuwakumba baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Kwa Zena, Block K.
Kamera ya Global ikipita maeneo hayo leo
asubuhi, imejionea zoezi hilo likitekelezwa kwa kutumia gari la ‘tinga
tinga’ likivunja baadhi ya majengo yaliyojengwa kinyume na sheria mtaani
hapo likiwemo moja ambalo mmiliki wake aliyetajwa kwa jina moja la
Evans anadaiwa kuvamia eneo hilo na kuweka uzio kwa kujengwa ukuta, huku
ikidaiwa kuwa kuwa, mmiliki halali wa eneo hilo ni mwanamke mmoja
aliyetajwa kwa jina moja Halima.
Manispaa imesema kuwa, oparesheni hiyo
ya bomoabomoa ni endelevu kwa watu wote waliovamia maeneo kiholela ama
waliojenga kwenye maeneo ya wazi (open space) ambayo hayajapimwa na
mamlaka husika.
PICHA: DENIS MTIMA NA DEOGRATIAS MONGELA/GPL
Post a Comment