Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge muda huu kutoka Bungeni Dodoma.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. John Magufuli anaelezea
kuwa mambo yote vipolo atayatatua na kuifaya Tanzania kufikia malengo
yake.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na suala la Katiba mpya ambayo amekili kuachiwa kiporo hivyo ataifanyia kazi ilikuikamilisha.
Suala la Muungano anaahidi kulifanyia kazi na kulitatua.
Awali:
Baada
ya Rais kuingia Bungeni hali ilikuwa ni ya kelele na kuzomeazomea kwa
wabunge lakini upepo huo ulitulia..Wabunge wa Upinzani katika Bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Watanzania Wanazomea Bungeni mara baada ya
Kutangazwa Kuingia kwa Rais wa Zanzibar Mh Dk Ali Mohamed Shein.
Wanachopinga
wabunge hao wanadai hawamtambui Dk Shein Kama RaisHalali wa
Zanzibar.Hali hiyo ilianza pale Naibu spika alipomuita Mwanasheria Mkuu
wa Serikali Kutengua Kanuni ili Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wameze Kuongozana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh Magufuli wakati atakapokuja Kulihutubia Bunge na Kulizindua Rasmi
,Wabunge hao waliaanza Kupiga kelele Mara Baad ya Kutangazwa kuingia kwa
Spika wa Baraza la Wakilishi Zanziba, Makamu wa Pili wa Rais ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Pamoja na Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar..
Post a Comment