NA BASHIR YAKUB-
Ardhi inaweza kumilikiwa na
mtu zaidi ya
mmoja. Inaweza kuwa nyumba
au kiwanja. Vyote hivi vinaweza
kumilikiwa na mtu zaidi
ya mmoja. Kumiliki ardhi kwa
zaidi ya mtu
mmoja sio lazima
iwe kwa wanandoa. Inaweza kuwa
ndugu , marafiki , kikundi
cha watu kama wafanyabiashara, wana saccos, kikundi cha
michezo na aina
yoyote ya kikundi
cha kimaendeleo. Umiliki
wa ardhi kwa
pamoja unatofauti na
umiliki binafsi yaani umiliki wa mtu
mmoja mmoja. Tutaona tofauti
hizo na mambo
mengine ya msingi
kuhusu umiliki wa
pamoja.
1.AINA ZA
UMILIKI ARDHI.
Kwa kuangalia ardhi
katika mrengo wa
umiliki tunaweza
kusema kuwa ardhi
humilikiwa kwa namna
mbili. Kwanza umiliki
wa mtu mmoja
mmoja na pili
umiliki wa pamoja.
Huu ni ule
niliosema kuwa ni
mtu zaidi ya
mmoja.
Umiliki binafsi wa
ardhi yaani umiliki
wa mtu mmoja mmoja unatoa
haki kwa mmiliki
huyo kuitumia ardhi
bila kuhitaji ridhaa
ya mtu mwingine
yoyote. Anaweza kuuza, kuweka
rehani kama dhamana
ya mkopo, kutoa zawadi,
kupangisha na matumizi
mengine yoyote halali.
Atafanya yote haya
bila kuhitaji ridhaa ya
mtu mwingine yoyote.
Hii ni tofauti
na umiliki wa
ardhi wa
pamoja. Katika umiliki wa aina hii
mtu mmoja hawezi
kuuza, kutoa zawadi, kuweka
rehani kupangisha au
kuruhusu matumizi ya
ardhi kwa namna yoyote ile bila
ridhaa ya wengine. Kama
ni wawili basi
ridhaa itabidi itokane
na wawili lakini
pia kama ni
kumi, saba , watano au
zaidi basi ridhaa
yao wote itatakiwa
kabla ya kufanyika
kwa muamala wowote ule.
2. KUUZA
BILA RIDHAA YA WAMILIKI WENGINE.
Ikiwa ardhi inamilikiwa kwa pamoja kwa
maana ya kumilikiwa na mtu
zaidi ya mmoja na
ikatokea kuwa mmoja
kati ya hao wamiliki ameuza bila
ridhaa ya wengine
basi mauzo hayo
yanakuwa batili kwa
mujibu wa sheria. Hata
kama wamiliki wapo kumi
na labda tisa
ndio waliouza bila ridhaa
ya mmoja, bado
mauzo hayo yatakuwa
batili kwa kukosa
ridhaa ya huyo
mmoja. Na ifahamike
hapa kuwa ubatili
sio katika kuuza
tu bali pia hata kuweka
rehani, kupangisha, kutoa zawadi
na katika muamala
wowote wa kisheria ambao utafanyika.
3. KILA
MMOJA KUWA NA
HATI YAKE YA
UMILIKI.
Umiliki wa pamoja
wa mke na mme
kwa maana ya
wanandoa hutakiwa kila
mmoja kati yao
kupatiwa hatimiliki yake
inayojitegemea. Katika hili
hatimiliki haipaswi kuwa moja
bali kila mtu hutakiwa kuwa na
yake. Hata hivyo hati
hizo zote huwa
zinafanana kimaudhui. Muhimu ni
kujua kuwa mwanaume
anakuwa na yake halikadhalika mwanamke.
4. KUANDIKISHWA
KWA UMILIKI ARDHI WA
KIKUNDI.
Iwapo ardhi inamilikiwa
na kikundi basi
umiliki huo hutakiwa
kuwa umeandikishwa kwa
msajili wa hati. Uandikishwaji huu
ndio hutoa haki
ya kila mmoja
kuombwa ridhaa kabla
ardhi hiyo kufanyiwa
muamala wowote.
5. KURITHIWA KWA HAKI
YA UMILIKI YA MMILIKI
ALIYEFARIKI.
Inapotokea kifo cha
mmiliki mmoja kati ya
wamiliki wanaomiliki pamoja
ardhi, basi haki
yake ya umiliki huweza
kurithiwa na wale wanaotakiwa kurithi
mali zake. Wale
wanaotakiwa kurithi mali
zake ni pamoja
na wale aliowaandika
katika wosia kama ameuacha au kupatikana kupitia taratibu za
kisheria za usimamizi
mirathi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
Post a Comment