Rais Dk. John Magufuli
Umesema staili watakayoitumia ni tofauti na ile waliyoitumia wakati
Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alipozindua Bunge la 10 mwaka
2010 ya kutoka nje ya ukumbi kuonyesha kutotambua serikali yake.
Akizungumza na Nipashe katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana,
aliyekuwa Mnadhimu wa Bunge la 10 Kambi la Upinzani Bungeni, Tundu
Lissu, alisema safari hii hawatatoka nje ya ukumbi wa Bunge hata kama
hawamkubali Rais Magufuli, kwa kuwa ni wajibu wao kushiriki vikao vya
chombo hicho cha kuwakilisha wananchi.
“Sisi ni wabunge, tumo humu kwa ridhaa ya wananchi, tuna haki ya
kuingia bungeni, hivyo siku hiyo tutaingia lakini kitakachotokea tutajua
siku hiyo, bali haitakuwa kama walivyotuzoea tunatoka nje,” alisema na
kuongeza:
“Subira yavuta heri, bado siku tatu tu, Watanzania watajua msimamo wetu tukiwa ndani ya Bunge,” alisema.
Hivi karibuni aliyekuwa mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema,
Edward Lowassa, alisema hawatambui matokeo yaliyotangazwa naTume yaTaifa
ya Uchaguzi (Nec) na kumpa ushindi Rais Magufuli na kwamba
hawatashirikiana na serikali yake kutokana na kile alichoeleza kuwa
uchaguzi mkuu uligubikwa na wizi wa kura na kuporwa ushindi.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment