Taarifa kamili ya Rais Shirikisho la
Muziki Tanzania ya kumpongeza Magufuli
Ndugu wanahabari, leo
hii tarehe 12 Novemba 2015 nimekuiteni hapa Kwenye ofisi zetu hapa Mlimani City
kwa ajili ya mambo machache.
Nisingependa
kuwapotezea Muda wenu mwingi Maana Sasa tunaongozwa na kauli Mbiu ya Hapa Kazi
Tu hivyo ni bora tukae Muda mfupi na kwenda kuchapa Kazi Tu.
Ndugu wanahabari
nimekuiteni kutoa pongezi za dhati na kuunga mkono kasi aliyoanza nayo ndugu
Magufuli siyo tu ameonesha kutosha Kwenye Kiti bali amekuwa mtetezi wa
wanyonge.
Ndugu wanahabari
Ziara za Ghafla za Ndugu Magufuli siyo za kubezwa Ni za kupongezwa sana. Japo
kuna wenye roho mbaya na wasioitakia mema nchi yetu wanabeza maana wao walizoea
kubweteka na kufurahia wanyonge wakiteseka.
Shirikisho la Muziki
Tanzania tumeona matunda ya Rais Magufuli juzi amekwenda Muhimbili na Jana
tangazo limetoka kuwa mashine za MRI zimeanza Kufanya Kazi hili jambo si la
kubezwa hata kidogo bila jitihada binafsi za Ndugu Magufuli leo watanzania
wangeendelea kufa na kukata tamaa kwa kukosa matibabu.
Ndugu wanahabari
haikuwa rahisi kwa wakati Kama huu ambao Ni wa Kupanga serikali mpya bado Rais
ametoa Muda wa kwenda kuhakikisha wanyonge wanapata matibabu na huduma tuna
pongezi sana Ndugu Magufuli.
Wembe Ni ule ule
aendelee na Ziara hizo za kushtukiza maeneo mengi yana uozo azibe mianya ya
wakwepa kodi hasa Kwenye madini ambako tuna Mikatana mibovu iliyoingiwa na
wasio na Huruma, wizi na usafirishaji haramu wa madini, Ni Jambo la aibu
Tanzanite kwa wingi ipo Kenya na Afrika Kusini na kodi hatukupata ipasavyo na
kwingine kwingi Kama Kwenye mbuga za wanyama na utalii ambapo wanyama wanauwawa
kwa Faida ya wachache Jambo hili ni la kulivalia njuga na mengine mengi.. Kwa
kuziba mianya hiyo na kuleta maendeleo ya wote hakika hatutahitaji misaada ya wazungu..
Tupo tayari kufunga Mkanda kwa miaka hii mitano ili kuacha hazina kwa Taifa
letu lenye kila aina ya utajiri.
Jambo la kumalizia
tunamtakia afya tele na tunaahidi ushirikiano kwake Kwenye haki za wanamuziki
Kama alivyotuahidi pale Mlimani City vile vile Tunamuombea kwa Mungu apate
Baraza la Mawaziri dogo lenye ufanisi na kupunguza mzigo kwa serikali Kama
dhamira yake alivyoionesha Kwenye kuondoa safari za Nje vile vile Tunamuombea
kwa Mungu asiogope vitisho vya Chura Yeye anywe Maji. Maji Ni kuwaletea
maendeleo watanzania.
Hali hii ya kasi ya
Magufuli itawafanya Diasporas wote wakumbuke kuwekeza nyumbani maana Sasa
wanajua hazina zao zitakua salama maana mwadilifu anaongoza nchi. Naomba
nichukue nafasi hii kuwatoa hofu watanzania waishio ughaibuni kuwa nchi ipo
Salama na Dereva wetu kwa Sasa ni Makini kweli kweli.
Zaidi ya yote
ninapongeza wasanii wote walioshiriki Kwenye kampeni za vyama mbali mbali Sasa
kampeni zimeisha Ni Muda wa Kufanya Kazi tuwe wamoja.. Rais wetu Ni Magufuli
tuvunje Makundi kwani siasa siyo uadui Ni Muda wa kujiletea maendeleo yetu
wenyewe!
Ndugu wanahabari Sasa
Tunaandaa Mkutano Mkubwa wa Amani na Maandamano ya kuunga Mkono Hatua za
Magufuli kwa kweli tuna Imani naye na tunaamini Mungu atamuwezesha kuyatimiza
yote na kukata Kiu ya watanzania.
Nakutakieni Kazi
njema,
Wenu
Addo November
Mwasongwe
Rais Shirikisho la
Muziki Tanzania
Email addonovember@gmail.com
12.11.2015
Post a Comment