Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WILAYA YA KINONDONI YAKUMBWA NA ''BOMOABOMOA'' KUBWA


Hizi ni baadhi ya picha za bomoa bomoa katika eneo la tukio hapa Mwenge, wameenda katika maeneo menginie ikiwemo Tegeta.

Inaelezwa kwamba wakazi waliokuwa wanaishi katika eneo la hilo walitakiwa kuondoka mapema kwa amri ya Serikali kutokana na kwamba maeneo hayo sio sehemu rasmi kwa makazi hivyo nyumba zote zilizokuwa zimewekewa alama ya mkasi zimebomolewa.

Zoezi hili ni muendelezo wa bomoa bomoa katika maeneo yatakayohusika na ubomoaji huo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni eneo la Biafra.


Baadhi ya majengo yaliyokuwa na maduka yamebomolewa.


Zoezi hilo likiendelea katika eneo la Mwenge.


Baadhi ya Askari wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi wakati wa bomoa bomoa

 Hapa Mwenge opposite magorofa ya Jeshi kazi inaendelea, hasara ni kubwa, kazi imeanza saa kumi usiku mpaka sasa hivi kazi inaendelea.
Bomoabomoa hiyo inaendelea eneo la mwenge karibia na maghorofa ya jeshi, wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa hawakupewa taarifa kuwa bomoabomoa inakuja.

Wakazi wa eneo hilo walalamikia hasara kubwa iliyowakumbwa, washindwa kuokoa vitu vilivyoko ndani.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top