Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo
ya Nje wa Italia, Mhe. Dkt. Mario Giro ambaye yupo nchini kwa ziara ya
kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 5 Februari, 2016, ambapo alitembelea ofisi za Wizara kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe.
Dkt. Mario Giro akizungumza na Mhe. Dkt. Susan Kolimba ambapo katika
mazungumzo yao walijadili uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo
hasa katika sekta ya uchumi na kusisitiza juu ya suala la kukuza na kuendeleza sekta binafsi. Pia nafasi ya Italia katika kusaidia sekta ya elimu ambapo kwa upande wa Tanzania nchi hiyo imekuwa ikitoa ufadhili kwa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT)
Kushoto ni Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia, Dkt. Raffaelle De Lutio na Balozi wa Italia nchini Mhe. Luigi Scotto ambao waliambatana na Mhe. Dkt. Mario Giro.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Innocent
Shio (kushoto) kwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara Bi. Mingi Kasiga ( wa pili kushoto) wakiwa na Bi. Olivia Maboko, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri wakifuatilia mazungumzo
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo
Balozi Innocent Shio akijadili jambo na Mhe. Dkt. Mario Giro huku Mhe. Kolimba na Bi. Kasiga wakishuhudia.
Post a Comment