Mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa (kushoto), mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mkapa Foundation, Balozi Charles Sanga wakiwasili katika sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilioambatana na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower.(Picha na Zainul Mzige)
Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ameuchangia mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa (Mkapa Foundation), Milioni 210 ili kuiwezesha kuzidi kutoa huduma bora kwa jamii.
Mohammed Dewji ametoa kiasi hicho cha pesa akiwa kama mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamini Mkapa (Mkapa Foundation) ambapo Milioni 200 imetolewa na Taasisi ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation) na Milioni 10 imetolewa na MeTL Group.
Akitoa hotuba katika sherehe hiyo, Mohammed Dewji amesema kuwa ametoa msaada huo ili kuiongezea nguvu Taasisi ya Benjamin Mkapa (Mkapa Foundation) katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ya Watanzania.
Alisema kuna changamoto nyingi nchini ambazo zimekuwa zikijitokeza na ili kukabiliana nazo zinahitajika taasisi kama ya Benjamin Mkapa ili ziweze kusaidiana na Serikali na ili waweze kutatua changamoto hizo zinahitajika sekta binafsi kusaidiana nao kukabili changamoto hizo.Nimekuwa mstari wa mbele kusaidia sehemu ambazo zinaonekana kuwa na mahitaji na changamoto nchini zipo nyingi haina jinsi inabidi kushirikiana ili kupambana na changamoto hizo,” alisema Dewji.
Aidha Rais na Mkurugenzi Mkuu huyo wa MeTL Group aliyataka mashirika binafsi mengine kuungana kwa pamoja na kusaidia kumaliza changamoto zilizopo nchini kwani anaamini kuwa wana nafasi kubwa kukabiliana na matatizo hayo na kuweza kuyamaliza. Nae mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa alimshukuru Mohammed Dewji kwa msaada ambao amewapatia na anaamini ni mmoja wa watu wa kuigwa nchini kutokana na misaada ambayo amekuwa akiitoa nchini kwa kupitia taasisi yake ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation). “Mohammed Dewji ni mfano wa kuigwa nchini na ameweza kuboresha biashara ya Tanzania kimataifa, ninaamini utadumu kwa kipindi kirefu zaidi na kuwa balozi mzuri wa Tanzania,” alisema Mkapa.Katika sherehe hizo za kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, kulifanyika harambee ambapo jumla ya Bilioni moja na Milioni mia moja na sabini zilichangishwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dk. Ellen Mkondya Senkoro akitoa historia fupi ya taasisi hiyo kwa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mkapa Foundation, Balozi Charles Sanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa neno katika sherehe za miaka 10 ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Mkapa zilioenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko huo.
Msaidizi mwandamizi katika utawala wa Kampuni ya MeTL Group, Shemane Amin pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad wakiwa kwenye dakika moja ya ukimya kumkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa wakati wa sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.
Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza kwenye sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.
Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kulia) akijiandaa kukabidhi zawadi ya picha kwa Mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakati wa sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.
Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha iliyoandaliwa na wafanyakazi pamoja na bodi ya Mkapa Foundation, Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakati wa sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo zilizoambatana na harambee ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo ambapo jumla ya shilingi bilioni moja na milioni mia moja sabini zilichangishwa.
Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi tuzo Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa ya kutambua mchango wake wa kuleta matumaini kwa watu wenye mahitaji na kuthamini maono na muongozo kama mwanzilishi wa taasisi ya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 kwenye sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo iiliyoambatana na hafla ya harambee kwa ajili ya kuchangia taasisi hiyo.
Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji na Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa kwa pamoja wakizundua jina jipya ambalo ni Mkapa Foundation -"Bringing HOPE to the Underserved".
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla ya miaka 10 ya Mkapa Foundation ilyoambatana na harambee ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo.
Post a Comment