Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

JE WAJUA CHANZO, DALILI NA TIBA YA UGONJWA WA KISUKARI ?

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell Disease).

Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya 2013, inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo ulimwenguni, yakifanya asilimia 63 ya vifo vyote kwa mwaka. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua watu zaidi ya milioni 36 kila mwaka. Asilimia 80 ya vifo vinasababishwa na magonjwa hayo hutokea nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo. Inakisiwa kuwa mwaka 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.

Nchini Tanzania, katika mpango wa upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dar es Salaam, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebaini kuwa idadi kubwa ya wanaume wanapatwa na magonjwa hayo kuliko wanawake. Uchambuzi huo umeonyesha magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na saratani zote ambazo zimekuwa chanzo cha vifo hivyo, huku serikali ikisema imeamua kuongeza juhudi za makusudi kupambana nayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mfuko wa Bima ya Afya, athari ya magonjwa yasiyoambukiza ni mara nne zaidi ya watu waliopo mijini kuliko vijijini, huku asilimia 12.8 ya wanaougua wakiwa wako mijini na asilimia 3.1 wako vijijini kutokana na mfumo wa maisha.

Uchunguzi mwingine uliofanywa na jopo la madaktari bingwa kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 ulibaini asilimia 79 ya watanzania wazee waligundulika kuugua magonjwa ya kisukari, macho na shinikizo la damu. Pia walidai magonjwa hayo yamekuwa kikwazo cha maendeleo kutokana na kuwasumbua wazee na hata wenye umri wa kati ya miaka 40 na 50.

Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya katika kundi hili la magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Watu milioni 285 duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni pia ikishika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo duniani.

Nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye kisukari ni China wagonjwa milioni 43.2, India wagonjwa milioni 40.9, Marekani wagonjwa milioni 25.8, Urusi wagonjwa milioni 9.6 na Brazil wagonjwa milioni 6. Nchi zenye idadi kubwa ya watu wazima wenye kisukari ni Nauru kwa asilimia 30, Bahrain kwa asilimia 25.5, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa asilimia 25, Saudi Arabia kwa asilimia 23.7 na Mauritius kwa asilimia 20.

KISUKARI NI NINI HASWA?

Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).

Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.

Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

TAKWIMU MBALIMBALI ZA UGONJWA  WA KISUKARI

Kulingana na ripoti mbalimbali karibu watu milioni 316 ulimwenguni pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu, ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu hawatambui kama wana tatizo hilo. Ingawa asilimia 8.3 ya watu watu wa Marekani wana Kisukari ambayo ni sawa na watu milioni 25.8 na kufanya Kisukari cha 7 kusababisha vifo vya watu Marekani.

Mamilioni ya watu wana ugonjwa huo lakini hawana habari! Ni ngumu zaidi kutibu ugonjwa wa kisukari kwa kuwa mtu anaweza kuishi nao kwa muda mrefu kabla haujagunduliwa. Hiyo ndiyo sababu watu husema kwamba ugonjwa huo huua kimyakimya.

NINI CHANZO HASA CHA KISUKARI?

Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucosi ambayo ni chanzo cha nishati/nguvu mwilini huingia katika damu. Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (Pancrease) kutengeneza kichocheo cha insulini. Kazi ya insulini ni kuondoa glucosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumika kama nishati.

Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo, huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insini kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.

Main Symptoms of Diabetes FikraPevu.com
Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.

Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo.

Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari. Ndiyo sababu kabla ya kuvumbua njia bora za kupima ugonjwa huo, mbinu moja ya kutambua kama mtu ana ugonjwa wa kisukari ilikuwa kumwaga mkojo wa mgonjwa karibu na kichuguu cha sisimizi. Ikiwa sisimizi wangevutiwa na mkojo huo basi hilo lilimaanisha kwamba mkojo una sukari.

NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?

Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:-

– Wenye uzito uliozidi,

– Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,

– Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

– Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,

– Wenye shinikizo la damu,

– Wenye msongo wa mawazo na

– Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara.

Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.

Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.

Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

~ Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
~ Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
~ Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
~ Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
~ Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
~ Wanawake kuwashwa ukeni.
~ Kutoona vizuri.
~ Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
~ Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
~ Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
~ Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
~ Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
~ Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.

FAHAMU MADHARA YA KUPIGA PUNYETO KWA MWANAUME

 UKOSEFU  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.

 Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.
Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:


  1. Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema
  2. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )
  3. Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )
  4. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini
  5. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema
  6. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.


Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume. Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka.

Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

  • Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.
  • Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA)


Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

  • Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume
  • Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :


  1. Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.
  2. Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana.  Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.



  • Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

  • Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.
  • Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame
  • Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa
  • Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume


DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO

Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

  • Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
  • Uume kurudi  ndani
  • Uume  kusimama  ukiwa  legelege
  • Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Huu Ndio Utajiri Mkubwa Utakaoupata, Kama Utaamua Kufanya Biashara Hii.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani.

Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.

Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.

Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira, ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

BAJETI YA SERIKALI NA MIPANGO YA WAPINZANI



Chambi Chachage


Tunajenga nyumba moja sasa tunagombania fito za nini? Swali hilo litokanalo na msemo maarufu nchini Tanzania linaweza kutumika kuelezea ukakasi uliojitokeza kuhusu Bajeti ya Serikali. Wabunge machachari waliozuiwa kuendelea na vikao vya Bunge la Bajeti wameamua kutafuta vilinge vingine. Huko nako wapo waliozuiwa.

Wadadisi wa mambo tunaamini ni haki ya Kikatiba kwa mtu yeyote kujadili masuala yoyote yaliyo muhimu kwa Taifa. Wasiwasi wetu ni kuwa ushabiki wetu wa kisiasa kuhusu sintofahamu inayoendelea kati ya Serikali na baadhi ya wapinzani inaweza kutufanya tukose utulivu wa kuchambua ni nini hasa wanachopingana kuhusu bajeti. 

Hivyo basi, tumeamua kuchukua fursa hii kuupitia ‘Uchambuzi wa Bajeti Ya Serikali 2016/2017’ uliopangwa kutolewa kwa Umma na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, katika kongamano lao lililozuiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 12 Juni 2016. Lakini kwa kuwa tunaamini kuwa mtazamo wa kiuchumi wa Waziri wa Fedha, Dakta Philip Mpango, una ushawishi mkubwa kibajeti basi uhakiki wetu hauna budi kurejea na kulinganisha taarifa nyingine muhimu za wizara yake.

Katika uhakiki wetu, uliojikita kwenye sekta za kilimo na viwanda, hoja yetu kuu ni kwamba kuna ‘miingiliano tata’ na ‘migongano hewa’ kati ya mipango ya maendeleo ya Serikali iliyotumika kuandaa bajeti na makusudio ya uchambuzi wa wapinzani wanaojitanabahisha kama wazalendo wanaofuata ‘Ujamaa wa Kidemokrasia’.

Uchambuzi wa Kiongozi wa wazalendo hao, kwa mfano, unakubaliana na Serikali kuhusu kujenga viwanda. Tena unaipongeza “sana” bajeti yake ya sasa kwa kulenga  “kuondoa changamoto ya miundombinu kwa kiwango kikubwa sana.” Lakini unadai kwamba: “Miundombinu inaweza kujengwa lakini ikawa haina watu wa kuitumia wala bidhaa za kusafirisha kwa sababu hakuna vivutio vya kuanzisha viwanda pia.”

Pamoja na kujaribu kuihuisha misingi ya Azimio la Arusha kuhusu sekta ya Umma kupitia Azimio la Tabora, wazalendo hao hawatofautiani sana na Serikali  kuhusu nafasi nyeti/tete ya sekta binafsi. “Ikumbukwe kuwa Serikali haianzishi viwanda”, uchambuzi wao unasisitiza, “bali inajenga mazingira mazuri ya wawekezaji kuanzisha viwanda.” Hivyo, unadai kwamba bajeti hii ya Serikali “haijaweka hivyo vivutio vya kuanzisha viwanda na ime­minya uwezo wa walaji kutumia kwa kudhibiti matumizi na pia kutoza kodi nyingi zinazopunguza uwezo wa kutumia bidhaa na huduma.”

Njozi ya wazalendo hao ni kuona wananchi wengi wakiwa na ajira zenye tija. Ila wanajua “viwanda vinachangia asilimia 20 ya ajira zote rasmi nchini na kwamba theluthi mbili ya Watanzania wameajiriwa na sekta isiyo rasmi.” Hivyo, wanaona “juhudi za kuongeza uzalishaji viwandani ni muhimu sana ili kuwaondoa Watanzania wengi kutoka sekta isiyo rasmi na kuwaingiza kwenye sekta rasmi.” Ndiyo maana kiitikadi hawaoni shida kuipima Serikali kwa “kutazama hatua mbalimbali za kisera [za] kuwezesha sekta binafsi kufungua viwanda vingi zaidi nchini na kuajiri watu wengi.’

Tathmini yao inawafanya wadhani kwamba “Serikali ilipaswa kuja na Sera mahususi za kufikisha asilimia 10 au zaidi ukuaji wa uzalishaji viwandani.” Ili kufanikisha hilo wanadai “Serikali haina budi ku­kaa na wenye viwanda na kupata mwafaka wa namna bora ya kuweka sera mahususi zitazopelekea uwekezaji mkubwa wa wenye mitaji katika viwanda na kuongeza uzalishaji.” Yaani hawajaridhika na maneno haya ya Dakta Mpango: “Bajeti hii imezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau mbali mbali wakiwemo wenye viwanda, wafanyabiashara na wengine wengi”? Wanataka ‘manahodha wa viwanda’ wawe na sauti zaidi? Mtazamo wa kiuchumi wa Kiongozi wao usiopingana dhahiri na ‘dhana ya kibepari’ ya mapinduzi ya viwanda yatokanayo na mapinduzi ya kilimo umepelekea uchambuzi wao pia udai kwamba:

“Kwa Uchumi wa Tanzania, ujenzi wa Sekta ya Viwanda hauwezi kufanikiwa bila kukua kwa sekta ya kilimo. Kilimo ndio sekta Kiongozi katika kutokomeza umasikini kwani inachangia theluthi moja ya Pato la Taifa na kuajiri theluthi mbili ya Watanzania wote. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano imeshindwa kufungamanisha Sekta ya Kilimo na ndoto ya maendeleo ya Viwanda. Ushahidi wa kisayansi unaotokana na Taarifa za Serikali yenyewe unaonyesha kuwa hakuna mahusiano kati ya mipango ya maendeleo ya viwanda na mipango ya maendeleo ya wananchi. (Uk. 5).

‘Dongo’ hilo ni zito hasa ukizingatia kuwa katika Hotuba yake ya Kufungua Bunge ambapo alimsifia Kiongozi huyo kwa ukomavu wa kisiasa, Rais alinena haya:

“Sura ya kwanza ya viwanda tunavyovikusudia ni vile ambavyo sehemu kubwa ya malighafi yake itatoka ndani, hususan kweye sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, na madini – na maliasili nyingine. Viwanda vya aina hii vitatupa fursa ya kujenga mfumo wa uzalishaji ndani ya nchi uliofungamana na kushikamana. Viwanda vya aina hii vitahitaji na kutegemea malighafi toka kwa wazalishaji wa sekta nilizozitaja, na kwa kufanya hivyo wazalishaji hao watakuwa na soko la uhakika humu humu ndani ya nchi.” 

Eneo mojawapo ambalo Bajeti kuu imejaribu kuzingatia alichosema Rais ni hili lilipo katika hotuba ya Dakta Mpango:

“Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwenye mafuta ghafi ya kula (crude edible oil) yanayotambulika katika HS Code 1511.10.00 kwa mwaka mmoja. Hatua hii inalenga katika kuhamasisha kilimo cha mbegu za mafuta hapa nchini na kukuza viwanda vya kutengeneza mafuta ya kula. Aidha, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati maalum wa kuendeleza viwanda vya kuzalisha mafuta yanayotokana na mbegu zinazozalishwa hapa nchini na kutumia fursa [ya] soko kubwa lililopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania inayo nafasi ya kuweza kuongeza uzalishaji wa mbegu za mafuta” (Uk. 87).

Mpango wa Maendeleo Wa Miaka Mitano unapopelekea sasa kinachodaiwa kuwa ni asilimia 1 tu ya Bajeti ya Maendeleo iende kwenye kilimo, je, ni kwa sababu ‘vipanga’ waliouandaa hawaelewi muingiliano wake na viwanda? Je, ni kwa sababu huko serikalini kuna ‘vilaza’ wa uchumi wa “viwanda vya kusindika mazao ya kilimo (agroprocessing industries)” ambavyo uchambuzi wa wazalendo hao unavipigia chapuo?

Serikali ‘sikivu’ ya Rais Magufuli inajua fika inachotaka kukifanya kiuchumi hata kama kuna dalili zinazoonesha kwamba haielewi kikamilifu inakoelekea na athari zake kwa undani. Kama wadadisi tulivyowahi kugusia hapo awali kuhusu ‘Dakta Mpango na Hatma ya Kifedha, Kibajeti na Kiuchumi’, njozi yake imejikita katika ujenzi wa mkusanyiko wa viwanda vilivyojikita katika kile ambacho ‘wachumi wa kiliberali’ wanakiona ni fursa ambazo uchumi wa nchi/jamii fulani unazo kuzidi washindani wake.
 
Ukiirejea taratibu ‘Taarifa ya Hali ya Uchumi 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17’ aliyoiwasilisha Bungeni tarehe 8 Juni 216, kwa mfano, utakutana na mkakati wa “kuanzisha kongane za viwanda (Industrial Clusters) za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo.” Hilo limejikita katika dhana ya ‘Minyororo ya kuongeza Thamani (Value Chains)’. Na ndiyo maana hotuba yake ya ‘Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2016/17’ inasema:

“Serikali hadi sasa imeipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania mtaji wa shilingi bilioni 60. Aidha, katika hatua za awali, benki imeainisha minyororo 14 ya thamani ya mazao ya kilimo katika sekta ndogo ndogo nane itakayopewa kipaumbele katika kutoa mikopo kwa kuanzia. Sekta hizo ni za uzalishaji wa nafaka; mifugo; ufugaji wa samaki, kilimo cha matunda, maua, mbogamboga, na viungo; mazao ya viwanda hasa miwa na korosho; mbegu za uzalishaji mafuta ya kula; na mazao ya misitu hasa ufugaji wa nyuki na mazao yake… kwa mwaka 2016/17, Benki imepanga kuendelea kutoa mikopo kwa angalau minyororo 14 ya thamani (agricultural value chains) itakayofanyiwa tathmini yakinifu kama iliyoanishwa kwenye mpango kazi wa kwanza wa 2016-2020” (Uk 27 & 53).

Suala la kilimo kwenye bajeti na mipango ya Serikali linazidi kutazamwa kwa jicho la kibiashara/kiwekezaji. Ndiyo maana katika hotuba hiyo hiyo Dakta Mpango anatujulisha kwamba madhumuni makuu “ya kuanzishwa benki hii ni kusaidia upatikanaji, utoshelezi na usalama wa chakula endelevu nchini na kusaidia katika kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha biashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.” Picha hii inaakisi maneno haya yaliyopo katika ‘Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17’:

“Mradi [wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Biashara] unalenga kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. Katika mwaka 2016/17 zimetengwa shilingi bilioni 1.227 fedha za ndani kwa ajili ya: kuendelea kutafuta fursa nafuu za biashara na masoko kwa bidhaa za kilimo na viwandani kupitia majadiliano baina ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa” (Uk. 92).
 Usuli huo unaweza kutusaidia kuelewa ni kwa nini Dakta Mpango alisema haya Bungeni: “Bajeti hii pia inalenga kujenga mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuwekeza ili kuvutia ushiriki wa wawekezaji wa ndani na nje katika kuendeleza viwanda na kilimo.” Hakika mpango wa Serikali ya Magufuli siyo kujenga lile Taifa la wakulima na wafanyakazi. Ni wa kujenga hili Taifa la wafanyabiashara na wawekezaji.

Viwanda vilikuwa viwe vya wafanyakazi na kilimo kiwe cha wakulima enzi hizo za Ujamaa. Ila enzi hizi za Uliberali viwanda vinatakiwa kuwa vya wawekezaji na kilimo kuwa cha wafanyabiashara. Kama hatuamini hebu tutafakari haya maneno ya Dakta Mpango wakati anawasilisha bajeti Bungeni: “Mheshimiwa Spika, azma kuu ya Serikali ni kuimarisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa mtazamo wa kibiashara, kukuza viwanda na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na sekta hii.”

Dakta Mpango anaonekana amechoshwa sana na tija ndogo na kipato kidogo katika kilimo. Sasa anatoa wito kwamba watu watumie “nguvu” na “ubunifu” wao “katika kilimo cha mazao ya thamani kubwa.” Ndiyo maana anataka “mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kijungujiko (subsistence farming) kwenda kilimo cha kibiashara.”

Je, mapinduzi hayo yanawezekana bila kuondoa idadi kubwa ya wakulima kwenye ardhi/mashamba yao ili kuwapisha wenzao wachache wanaoonekana kuwa wabunifu zaidi na wenye mtazamo wa kibiashara/kijasiriamali? Kama ni kweli kilimo kinaajiri zaidi ya asilimia 70 nchini kama Dakta Mpango anavyodai, je, lengo hasa la mipango na bajeti ya Serikali ni kuhakikisha watu wote hawa wanabakia kwenye sekta hiyo?

Cha kushangaza ni kwamba swali hili la msingi katika stadi za maendeleo ya uchumi  haliguswi au linapotezewa tu. Kwa mfano, Kiongozi wa ACT-Wazalendo anasema: “Kwa sisi wachumi tunatambua kuwa ili kupunguza umasikini wa Tanzania kwa zaidi ya nusu ilihitajika sekta ya Kilimo kukua kwa kati ya asilimia 8 na 10 kwa mwaka. Kwa ukuaji huu tulionao sasa, maana yake itachukua miaka mingi sana watanzania kuondoka kwenye dimbwi la umasikini. Baadhi ya mazao yanayotarajiwa kuzalisha malighafi za viwanda uzalishaji wake umeporomoka kwa kiwango cha kutisha.”

Rai hiyo ya Wazalendo haiiambii Serikali inawezaje kukuza sekta kwa ‘mwendokasi’ huo bila hata kuwa na mbadala kwa wakulima watakoachwa. Inachoambulia kupewa ni mapendekezo yanayolenga “kumwezesha mkulima kubakia na sehemu kubwa ya mapato yake na kuvutia wananchi wengi kujishu­ghulisha na uzalishaji katika kilimo.” 

Ombi letu wadadisi ni kujibiwa hili tu: Tanzania ya viwanda ni Tanzania ya kilimo?
 
CHANZO:UDADISI 

LEE MUTUZZZ :JE UNA MAPANGO WA KWENDA KUSIHI MAJUU ?

Leo i want to touch this very sensitive subject ya wanaodai kuwa inapokuja kwenye diaspora huenda nina wivu na chuki na wanaoishi majuu kwa sababu nilirudi, ha! ha! ha! kwa wale ambao hamjafika majuu naomba kusema hivi:- mungu alinijalia sana confidence in myself na everything i do, nilipofika majuu kwa mara ya kwanza nilikuta wabongo karibu wote pale New York wanafanya kazi za kulinda na kutunza wazee na mataharia, siku moja mbongo mmoja alinipeleka kwenye kazi ya kutunza mataahira nilikaa kama lisaa limoja tu sikurudi tena, nikaenda shule kutafuta leseni ya cdl ya kuendesha malori makubwa sana ambayo hapa bongo hayapo, kazi ambayo inalipa haswa nikahangaika mpaka nikapata ile leseni nikiwa ninafanya kazi gas station mchana na usiku Kentucky Fried Chicken. Nilipopata leseni nikaanza kuendesha malori America nzima. Wale wabongo niliowakatalia zile kazi zao wakaanza kunizushia maneno kwamba ninauza unga, ha! ha! ha! ha!,

Kabla ya kwenda New York nilishakuwa baharia Belgium so Ulaya haikuwa kitu kigeni kwangu, ndio maana siku moja nikaamua kurudi Bongo mwenyewe bila kulazimishwa na mtu. Cha kwanza nilipofika tu bongo nikaanza kunenepa, why? Kwa sababu ni kwa mara ya kwanza katika miaka 30 ya maisha yangu nimeweza ku-relax na maisha. Majuu ni kufanya kazi tu na kulipia madeni, wazungu sio wajinga wameitengeneza system yao to the point wewe unaenda kuchangia uchumi wao tu hauwezi kuwa tajiri maana uwezekano haupo, wewe ni kazi tu, social life hamna ni kazi tu kila ukikaa unawaza kazi, mabebez hamna, wachache wabongo waliopo ni hasara tupu wengi wao hawajitambui. Kwenye uzungu hawapo kwenye ubongo hawapo wapowapo tu ole wako uwaguse, i mean kila kitu majuu ni perfect lakini gharama yake haikupi nafasi wewe kuwa na pesa extra, ndio unagundua kwamba majuu sio kama ulivyotegemea maisha ni mazuri lakini magumu sana kurudi bongo nako huwezi maana ni noma zaidi so you are stuck, i was stuck too mpaka nilipoamua kwa hiari yangu kurudi home.

Hapa sina deni kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, sidaiwi na mtu kila nilichonacho, kama ni gari ni langu, apartment ni yangu, shamba na nyumba ni vyangu sidaiwi na mtu, nafanya kazi ya kujiajiri, nakuja kazini saa ninayotaka, ninatoka saa ninayotaka, kwa mara ya kwanza ninamiliki simu za usd $ 1000 a piece majuu ningekuwa nayo ya kukopa na sikuwahi kuwanazo, bongo maisha baada ya kazi hayana mfano, marafiki kila kona kule unakuwa huna marafiki, bongo heshima kila kona majuu mweusi atakuheshimu nani? i mean kwenye kujiajiri nikipiga deal moja ikaitika millions zinakuwa zangu sio kulipia madeni, ninasafiri bongo na nje ya bongo anytime i want majuu nisingeweza maana ni kazi tu all the times.

Sasa naomba kuuliza jamani kweli niwaonee wivu na chuki waliobaki majuu kwa kisa gani? nasema hivi majuu wanatuzidi bongo kwa one thing matibabu wao wakiumwa kule ni rahisi sana kupona kuliko hizi hospitali zetu bongo, ni hilo tu mengine hapana bongo kuna maisha asikudanganye mtu, again mungu alinijalia moyo wa kujali yangu zaidi na sio ya wengine so kwa wale mnaolia lia kwamba nawaonea wivu eti mko majuu ha! ha! ha! ha! please!!, ninafanya biashara na wabongo wengi huko nje inapokuja kwenye kulipa ni kivumbi na patashika lakini hapa bongo ni tofauti watu wanalipa mara moja tena mpaka kwa dola za kimarekani, jamani kwa wale ambao hamjafika huko majuu na unaweza kula milo mitatu bongo bila tatizo tulieni hapa hapa jamani huko majuu kusikieni tu!!, ninamshukuru mungu kila siku kwa kunipa akili ya kwenda majuu na pia ya kurudi home ontime kabla sijachelewa, ndugu zangu huko rudini huku bongo maisha ni sawa ila tu ujipange kabla ya kuja na muhimu kuliko yote soma shule kwanza, huku bongo bila elimu utachekesha maana hela ukijanazo zitaisha kama huna elimu. jamani samahani kwa maelezo marefu lakini i hope nimemsaidia somebody out there!! - Le mutuz.

MADEREVA DALADALA NA 'HATI MILIKI YA BARABARA ZA JIJI'


Huku mradi wa Mabasi ya mwendo kasi ukisubiriwa kwa hamu Jijini Dar es Salaam wengi wetu tumekuwa tukijiuliza maswali mengi mojawapo likiwa hizi daladala kweli zitauacha mradi huuu salama ?

Madereva daladala wamekuwa wakiendesha kama vile wana hati miliki ya barabara zote za jiji la Dar es salaam,hawajali watumiaji wengine wa barabara hizo.

Iwe kwa madereva wengine wa gari ndogo au watembea kwa miguu,madereva wa daladala wao hujiona ndio wenye miliki ya barabara.

Shaka yetu imejidhihirisha pale daladala moja lilipovamia njia ya Mabasi ya Mwendo kasi na kuligonga basi mojawapo maeneo ya magomeni mapepa.

HANS POPPE AMJIA JUU JERRY MURO

Wakubwa wanapogombana ujue kuna jambo haswa wakubwa wenyewe zikiwa ni klabu kongwe nchini Simba na Yanga.
 
Wote wanajuana nje na ndani ya uwanja.Namna timu hizi zinavyofanya fitna ili ziweze kupata matokeo mazuri katika mechi zao za Ligi lakini mara wanapofika katika mechi za kimataifa hali huwa tete sana mara nyingi huishia raundi ya pili.
 
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,Zacharia Hans Poppe ametoa mwanga kidogo kwa yale yanayofanyika kwa wakongwe hao wa soka nchini.Akimshutumu Msemaji wa Yanga Jerry Muro.
 
HIVI NDIVYO ALIVYOHOJIWA NA GAZETI LA CHAMPIONS:
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema ameshangazwa na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro kujishitukia baada ya yeye kusema mwishoni mwa ligi, kuna michezo ya rushwa na akaitaja aina yake.
 
 


Hans Poppe amesema ameona Muro akihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusema anataka kumpeleka Takukuru ili akaeleze kuhusiana na rushwa.



“Lakini kinachonishangaza ni kitu kimoja, mimi sikutaja jina la mtu wala timu. Utaona nilifanya mahojiano na gazeti la Championi, hata ilivyoandikwa sikutaja klabu wala jina la mtu, sasa unapomsikia mtu wa sehemu fulani anakurupuka na kusema kitu, huoni hii ni hofu.



“Nimeshangazwa sana kusikia mtu anahojiwa, anajitaja, analalamika wakati hakuwa ametajwa mtu,” alisema Hans Poppe.



“Hii inanikumbusha mwaka 1978, Uganda walikuwa wanarusha ndege zao za kivita zinaingia hadi anga ya Tanzania. Rais Nyerere akasema kuna watu ambao ni majirani zetu wanarusha ndege zao zinaingia ndani ya enero letu, nafikiri wanatutafuta.



“Siku iliyofuata Iddi Amini aliyekuwa Rais wa Uganda wakati huo akasema, sio mimi. Sasa ndiyo anachofanya huyu kijana hapa,” alisema.




Hans Poppe alihojiwa na gazeti la michezo la Championi na kueleza kuhusiana na suala la rushwa.

UCHAFU BADO HALI SIO SHWARI JIJI DSM



Wengi tunatamani kuona miji yetu ikiwa misafi kama nchi ya Rwanda lakini bado hali hiyo imekuwa safari ndefu  kwetu kwani bado tungali tukiona mifuko ya lambo na viroba vikiwa vimejaa uchafu.

Kumekuwa na juhudi nyingi na matamko mbalimbali kufanikisha usafi lakini tumekuwa tukirudi kule kule kwa mwanzo(uchafu kila eneo).

Baada ya tamko la Mkuu wa MKoa wa Dar es Salaam,Mhe.Paul Makonda kuhamasisha usafi Jijini hali iliyoleta faraja kuwa sasa ile ndoto yetu kufanana usafi au kuwapita Rwanda imetimia.

Lakini katika pitapita katika maeneo mbalimbali bado hali sio tuliyoitazamia,usafi umefanyika lakini bado viroba na mifuko iliyojaa uchafu imezagaa. 


Tunajiuliza magari ya kusombea taka taka yapo wapi ?

Je hatukujianda na hili ?

HABARI YA MUJINI:Punguzo Kodi ya Mishahara Kwa Wafanya Kazi Laibua Mapya

Uamuzi wa Rais John Magufuli kupunguza asilimia mbili ya Kodi ya Mshahara (PAYE) umeibua mjadala baada ya kubainika kuwa utampa nafuu ndogo mfanyakazi, huku wachambuzi wakihamia kwenye kodi nyingine ya mapato kwa kuzingatia viwango vya mishahara.

Baadhi ya wadau wanapendekeza kodi hiyo, inayoitwa excess charge, ipunguzwe kumpa unafuu mfanyakazi, huku wengine wakishauri kuweka nguvu kwenye uchumi wa viwanda na kilimo na baadhi wakishauri juhudi zifanyike kudhibiti mfumuko wa bei ili mshahara utosheleze mahitaji ya mfanyakazi.

Baadhi ya wadau wanapendekeza kodi hiyo, inayoitwa excess charge, ipunguzwe kumpa unafuu mfanyakazi, huku wengine wakishauri kuweka nguvu kwenye uchumi wa viwanda na kilimo na baadhi wakishauri juhudi zifanyike kudhibiti mfumuko wa bei, ili mshahara utosheleze mahitaji ya mfanyakazi.

Juzi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Rais alitangaza kupunguza kodi ya PAYE kutoka asilimia 11 hadi tisa, lakini kwa mujibu wa wahasibu uamuzi huo ni punguzo la Sh1,100 kwa wafanyakazi wa mshahara wa kima cha chini na Sh3,800 kwa mshahara unaoanzia Sh360,000 na kwenda juu.

Akifafanua kuhusu PAYE, mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard Kayombo alisema kiwango cha mapato kisichozidi Sh170,000 hakina kodi, lakini mapato ya kati ya Sh170,000 hadi 360,000 yalikuwa yanakatwa asilimia 11 na hivyo sasa yatakatwa asilimia tisa.

Alisema mapato yanayoanzia Sh360,000 hadi 540,000 hukatwa PAYE pamoja na asilimia 20 ya excess charges, wakati mshahara unaozidi Sh540,000 hukatwa PAYE pamoja na asilimia 25 ya makato ya excess charges.

Suala hilo pia lilizungumzwa na mchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa, Godlisen Malisa katika waraka alioutuma kwenye mtandao kuchambua punguzo hilo la Rais Magufuli.

Malisa alionyesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kusifu punguzo hilo, wakiwamo wabunge wa upinzani.

“Kama Rais angepunguza excess charges, angalau zikafika 10% kutoka 30% ziliko sasa, ingekua na maana kubwa sana kuliko kupunguza PAYE,” anasema Malisa katika waraka huo.

“Kwa kifupi ni kuwa punguzo hilo litawanufaisha zaidi wenye mishahara chini ya 720,000/= lakini kwa wanaolipwa zaidi ya hapo hakuna benefit (manufaa) yoyote. Hata hao wanaolipwa chini 720,000/= bado watanufaika kidogo sana.”

Alidai kwamba kama kuna mbunge yeyote anayeshangilia punguzo ni wazi kuwa hajui hesabu, hivyo anatakiwa kukumbushwa ili aelewe kuwa kupunguza PAYE wakati makato yanayozingatia viwango vya mishahara yako palepale, ni kiini macho.

“Yaani Rais JPM alichofanya ni kutulazimisha tukatae ongezeko la mshahara,” anasema.

Alisema ni kweli wapinzani waliomba PAYE ipunguzwe tangu mwaka 2011 kwamba isomeke kwa tarakimu moja na ndivyo alivyoahidi JPM, lakini pia walishauri kuwa gharama za makato hayo ya zaidi yalingane.

“Nimeamua kusema hivi maana naona wabunge wengi wa (vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi) Ukawa wanacheza ngoma ya Magufuli. Wanaanza kujitapa (kwamba) upinzani tulishauri jambo hili tangu mwaka 2011,” anasema.

“Wengine wanapiga picha hadi hotuba ya kambi ya upinzani iliyozungumzia jambo hilo. Waambieni wakae kimya na wasiendelee kuongea vitu wasivyovijua.”

Mtaalamu wa masuala ya kodi, Dk Mariam Nchimbi alisema kiwango cha mshahara kingepandishwa ni wazi kingesaidia wengi kujipanga vyema, ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa kodi zinazostahili.

“Ni wazi kwamba kwa hatua hiyo ya Rais imewasaidia kwa kiasi fulani wale wanaolipwa mishahara ya kiwango cha kati, lakini wale wa kiwango cha juu pia walipaswa kupunguziwa japo kwa asilimia 28 badala ya 35 inayokatwa sasa,” alisema.

Lakini wachambuzi wengine waligeukia suala la kukuza uchumi wakisema ndilo litakalosaidia mfanyakazi kunufaika na mshahara wake.

Profesa Humphrey Moshi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema mshahara wenye nafuu kwa maisha ya wafanyakazi wengi utapatikana kutokana na uwepo wa viwanda vya kutosha pamoja na kilimo kuimarishwa.

“Kuna mambo mengi ya kuangalia ili mfanyakazi awe na mshahara ambao unampa unafuu wa maisha,” alisema Profesa Moshi.

“Pato la Taifa linahusika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama litajengewa mazingira ya kukua, itakuwa vyema. Inatakiwa viwanda vichangie pato hilo kwa asilimia 25 na si asilimia nane kama ilivyo sasa.”

Alisema anaamini baadhi ya viwanda hivyo vitakuwa vya kusindika mazao, kutakuwa na kilimo cha biashara ambacho kitaongeza tija.

“Ninaamini kuwa mbali na maeneo hayo, viwanda vingine vingi vinaweza kuendelezwa kama vya usindikaji mazao ya kilimo na uzalishaji ,” alisema.

Alisema kwa upande wa Serikali mshahara wenye nafuu ya maisha kwa watumishi wake unapaswa kujengewa mazingira labda kwa kuweka idara maalumu ambayo inaangalia viwango vya mishahara.

“Kwa ilivyo sasa ni wazi kuna watumishi ambao wananufaika kama alivyowahi kueleza Rais. Yaani watu wanalipwa mishahara kama wapo Ulaya. Sasa mfano unaweza kukuta mtu kaajiriwa hapa UDSM ni msomi kwa viwango, lakini analipwa Sh3 milioni wakati mwenye digrii aliye Benki Kuu analipwa Sh6 milioni,” alisema.

Profesa Moshi alihoji kwa viwango hivyo viwili tofauti, nini kimetumika kuamua mwenye elimu kubwa alipwe kidogo na mwenye elimu ndogo alipwe zaidi.

Alisisitiza kuwa Serikali inapaswa kuzibana bodi za taasisi zake ambazo zimejijengea mazingira ya kulipa mishahara ya mamilioni ya fedha bila kujali hali ya nchi kwa ujumla.

Msomi mwingine, Dk Ulingeta Mbamba kutoka Shule ya Biashara ya UDSM, alisema Serikali inabidi idhibiti mfumuko wa bei.

“Ni wazi kwamba hata kama Serikali itaongeza mshahara, bidhaa zikawa zinapandishwa kiholela, hakuna siku kiwango cha mshahara kinaweza kutosheleza maisha ya watumishi,” alisema.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top