Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TETESI ZA USAJILI SOKA ULAYA:ALVARO MORATA, GONZALO HIGUAIN NA MARIO GOTZE WAWINDWA NA WENGER


Manchester United wameongeza dau hadi pauni milioni 28 kumtaka kiungo wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan, 27 Gazeti la Mirror limeripoti hii leo ikiwa ni jitihada za Kocha mpya Jose Mourinho kuimarisha kikosi chake kabla ya msimu kuanza.Ambapo Manchester United wataanza kwa kukipiga na
Bournemouth wikiendi ya 13-15 Augusti 2016(SOMA HAPA:EPL KUANZA KUUNGURUMA 13/AUGUST/2016).Wakati huo huo Uamuzi wa Zlatan Ibrahimovic kustaafu soka la kimataifa baada ya Euro 2016 unamaanisha mchezaji huyo, 34, hatocheza michuano ya Olimpiki wakati EPL inaanza na hivyo kufungua njia kwa Manchester United kumsajili (Mirror)


Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 26, atapewa „mkataba wa maisha” na Real Madrid ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani (Daily Mail), Real Madrid kumsajili tena Alvaro Morata kutoka Juvenyus kunamaanisha Chelsea, Tottenham na Arsenal watapata nafasi ya kupanda dau kumsajili mchezaji huyo, 23, huku Real Madrid wakitaka kumuuza kwa faida kubwa (Times),

Manchester City wana matumaini ya kukamilisha usajili wa winga kutoka Ujerumani Leroy Sane, 20, kwa pauni milioni 40 ifikapo Jumatano, lakini mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich nao wanataka kupanda dau (Sun), mshambuliaji wa Spain na Celta Vigo, Nolito, 29, ameamua kujiunga na Manchester City kwa mkataba wa miaka mitatu (TV3).


Kiungo kutoka Brazil, Willian, 27, anajiandaa kusaini mkataba mpya Chelsea licha ya Manchester United kumnyatia (Sun).

Leicester wanakaribia kukamilisha uhamisho wa Nampalys Mendy, 23, kutoka Nice kwa pauni milioni 13 (Times)

Watford wamewaambia Leicester kuwa mshambuliaji wao Troy Deeney, 27, hauzwi (Daily Mail)

Romelu Lukaku, 23, huenda akasalia Everton, kwa mujibu wa wakala wake (Sportwereld), bilionea mpya wa Everton Farhad Moshiri anataka mchezaji ‘mkubwa’ kusajiliwa na yuko tayari kutoa mshahara mnono (Liverpool Echo).

Roma wamekuwa na mazungumzo na Manchester City kuhusu kumsajili beki kutoka Argentina Pablo Zabaleta, 31, ambaye mkataba wake unamalizika mwakani (Gazzetta dello Sport), Zabaleta pia anaweza kwenda Inter Milan kuungana na meneja wa zamani wa City Roberto Mancini (Telelombardia)


Winga wa Newcastle Andros Townsend, 24, hafuatiliwi na Liverpool, badala yake Jurgen Klopp anamtaka mshambuliaji wa Southampton Sadio Mane, 24 (Liverpool Echo), dau la Liverpool la pauni milioni 7 kumtaka beki wa kushoto wa Leicester Ben Chidwell, 19, limekataliwa (Telegraph).


Leicester City wamehusishwa na kumtaka mshambuliaji wa Juventus Simone Zaza, 25 (Leicester Mercury)

Meneja wa Swansea muitaliano Francesco Guidolin anamtaka pia Zaza (Sky Italia)

Kiungo kutoka Spain Mikel Arteta, 34, bado hajaamua iwapo anataka kujiunga na Pep Guardiola kama mmoja wa wasaidizi wake Manchester City, baada ya kuondoka Arsenal (Sky Sports).

Urusi wanataka Manuel Pellegrini kuwa meneja mpya wa timu ya taifa na wamempa mkataba mnono (AS)

Swansea wametoa dau la pauni milioni 2 kumtaka beki wa kati wa Ajax, Mike van der Hoorn (De Telegraaf). 

Hizi bado ni tetesi kwa hisani kubwa ya Daily Maily na Salim Kikeke
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top