Rais John Magufuli
Rais John Magufuli amesema Alhamisi kuwa anashangazwa na idadi ya vibali vya kusafiri nchi za nje vinavyoombwa na majaji na kuonya kuhusu likizo za nje ya nchi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania, Rais amesema vibali hivyo vinaonyesha majaji hao na familia zao wanasafiri kwa ajili ya likizo.
Akizungumza katika kilele cha Wiki ya Sheria Dar es Salaam Alhamisi, Rais amemwagiza Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma kufuatilia suala hilo.
Amesema amekuwa akijiuliza wanawezaje kugharimia likizo hiyo ya siku 28-30 wakiwa nchini Afrika Kusini, Uingereza na nchi nyingine wakati kipato chao anakijua.
Ameeleza kuwa wakati watumishi wengine hutumia siku za likizo kwenda vijijini kwa wazazi wao, lakini wengi wa majaji wanaochukua likizo huenda nje ya nchi kwa siku nyingi na amedadisi ni nani anayewagharamia.
Post a Comment