Sadio Mane alifunga hat-trick wakati Liverpool walipata ushindi mkubwa kwa kuwachabanga FC Porto 5-0
Sadio Mane alikuwa wa kwanza kutikiza wavu wa kipa Jose Sa kushindwa kuzuia mkwaju wa Mane.
Mohamed Salah akafuatia na bao la pili na lake la 31 tangu ajiunga na Liverpool hivyo kuipa Liverpool nafasi zaidi kusukuma mashambulizi mbele.
Mashambulizi ya counter-attack ya Liverpool yalisababisha Sa kuutema mkwaju kutokana na shambulizi lililofanywa na Mane baada ya kupata mpira safi kutoka kwa Roberto Firmino kabla ya Firmino kufunga bao lake la 21 kwenye msimu.
Liverpool waliwanyima Porto nafasi ya kuwashambulia kama ilivyokuwa imetazamimiwa.Porto imepoteza mechi mbili tu katika mashindano yote kabla ya mechi ya Jumatano lakini wakati huu ilishindwa kustahimili kishindo cha Liverpol kutoka kwa washambuliaji walionolewa.
Post a Comment