Usiku wa jana ulikuwa mzuri kwa baadhi ya mashabiki kutokana na miamba miwili ya soka Real Madrid na PSG kupepetana.Lakini macho yalikuwa kwa CR7 na Neymar kwani kila mmojawapo akishika mpira ilikuwa ni shangwe upande mmoja huku mwingine ukibeza hivyo kuufanya usiku kuwa mtamu sana kwenye vibanda umiza.
“Mtoto yake nepi” Real Madrid msemo huo umedhihirika baada ya usiku wa leo baada ya Real Madrid kutoka nyuma kwa bao 1 kwa 0 mbele ya PSG na kisha kuumaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao 3 kwa 1.
Cristiano Ronaldo aliweza isaidia Real Madrid kwa kufunga mabao mawili hivyo kuipa nafasi zaidi Madrid tumaini la kuingia robo fainali hivyo kuzidi kupata tumaini la kutetea taji lao miaka mitatu mfululilo.
Post a Comment