Bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB) imefanya marekebisho ya ratiba ya baadhi michezo ya ligi hiyo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushiriki wa vilabu vya Simba na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa.
Mchezo kati ya Simba dhidi ya Stand united uliokuwa uchezwe machi 4, 2018 umerudishwa nyuma hivyo utachezwa Machi 2, 2018 ili kuipa simba fursa ya kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao wa Caf Confederation Cup dhidi ya Al masry.
Mechi kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya yanga uliotarajiwa kuchezwa Machi 3, 2018 umeondolewa hadi hapo utakapopangiwa tarehe nyingine. Sababu ya kuondolewa kwa mchezo huo ni kuipa Yanga nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya mechi yao ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers
Mechi nyingine ambazo ratiba zake zimebadilishwa ni pampoja na Lipuli vs Ndanda mechi ambayo ilkuwa ikitarajiwa kuchezwa Machi 2, 2018 lakini imesogezwa mbele mpaka Machi 4 ili kutoa nafasiya kujiandaa kwa Ndannda ambayo itacheza kesho dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Nagwanda Sijaona, Mtwara. Kagera vs Mwadui mechi yao ilikuwa ichezwe machi 11, 2018 imesogezwa mbele hadi machi 13 ili kuipa nafasi mwadui.
Ligi itasimama Machi 22 ili kupisha mechi za kimataifa za kirafiki.
Post a Comment