Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Neymar ataukosa mcheoz wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid baada ya kuumia mguu.
Neymar alijiunga na PSG kwa uhamisho wa £200m kutoka Barcelona August,2017 na amefunga magoli 29 katika michezo 30 aliyocheza.
Haijulikani atakuwa nje kwa muda gani kutokana na kuumia huko.
PSG wana pointi 14 zaidi Monaco wanaoshika nafasi ya pili na tarehe 6 Machi wanawakaribisha Real Madrid, ambao wana mtaji wa mabao 3-1 kutokana na ushindi katika mchezo wa kwanza.
Post a Comment