Liverpool wanajiaanda kutuma ofa ya pili kwa Monaco kumsajili kiungo mchezeshaji mwenye umri wa miaka 22 Mfaransa Thomas Lemar,baada ya mchezaji huyo kukataa kandarasi mpya ya kuitumikia Klabu yake ya Ligue 1 . (Chanzo:Independent)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atarudi tena kwa Mualgeria Riyad Mahrez mwenye umri wa miaka 26 anayekipiga Leicester City's mwishoni mwa msimu . (Mirror)
Luis Enrique, Kocha wa zamani wa Barcelona ambaye amehusishwa na kumrithi Antonio Conte wa Chelsea, anajiandaa kuelekea Uingereza. Kocha huyo mwenye miaka 47 anataka kuchukua mikoba hiyo lakini iwe mpaka mwisho wa Msimu . (Telegraph)
Tottenham wanataka kumsajili Mfaransa Abdoulaye Doucoure mwenye Umri umri wa miaka 25 anayekipiga Watford . (Mail)
Mbrazil amabye ni beki Fabinho, 24, ambaye Manchester United walikuwa wakimnyatia msimu uliopita,amesema muda wake kuwa Monaco ukaribia mwisho "coming to an end". (Metro)
Klabu ya Chinese Super League Hebei China Fortune wanatayarisha ofa nyingine kwenda Barcelona kuweza kumpata Lionel Messi, 30, baada ya ofa ya kwanza kukataliwa . (Mundo Deportivo - in Spanish)
Nottingham Forest wanataka kumsajili kipa mgiriki Stefanos Kapino mwenye miaka 23 aliondoka Olympiakos - ilipokuwa ikimilikiwa na mmiliki wa sasa Forest Tajiri Angelos Marinakis baada ya kutokuelewana. (Sun)
Mshambuliaji Benik Afobe, 24, yupo mbioni kurudi Wolves moja kwa moja kama vinara hao wa Championship wataweza kuingia EPL. Aliondoka Molineux kujiunga Bournemouth Januari 2016 lakini alirudi kwa mkopo Januari. (Mirror)
Na Chediel Charles
Kwa msaada wa mitandao
Post a Comment