Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MENEJA ARSENAL ALAUMU USAJILI MBOVU

Arsenal walianza vyema mechi dakika za kwanza tano na pia wakakamilisha kipindi cha kwanza vyema Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan wakikaribia kufunga.
Waliwachezea wachezaji wawili wapya, Mgiriki Sokratis Papastathopoulos beki wa kati aliyetokea Borussia Dortmund, na kiungo wa kati kinda wa miaka 19 Guendouzi aliyekuwa akichezea Lorient ya Ufaransa.
Guendouzi alicheza vyema na anataraiwa kuchezeshwa zaidi na Emery Unai msimu huu.
"Ilikuwa mechi yake ya kwanza Ligi ya Premia. Ana sifa nzuri na ustadi pia na akiwa uwanjani ataimarika haraka zaidi," alisema meneja wa Arsenal.
Kulikuwa na dalili kwamba Arsenal ambao walicheza kwa mfumo wa 4-2-3-1 wanahitaji muda zaidi kuzoea mfumo huo mpya.
"Matokeo yalikuwa 2-0 lakini nafikiri kwa jumla katika dakika hizo 90 tulikuwa tunaimarika," Emery alisema.
"Kipindi cha kwanza hatukucheza tulivyotaka. Tulizungumza wakati wa mapumziko kuhusu kuwajibika zaidi kipindi cha pili, kujituma zaidi. Tulitaka tuimarisha udhibiti wa mpira na kuzuia pasi zao. Nafikiri katika kipindi cha pili tulicheza zaidi jinsi tulivyotaka."
Meneja huyo wa zamani wa Sevilla na Paris St-Germain alisema alifurahia mandhari Emirates.
"Tulitaka kuanza hapa na wafuasi wetu. Tulitaka kuonyesha ustadi wetu lakini ni wazi kwamba mikononi mwa Manchester City hatungeweza kuwapa (mashabiki) ushindi. Lakini nafikiri hapa mambo yatakuwa sawa sana."
Arsenal na Unai Emery walikuwa na ratiba ngumu ya mechi kwani sasa wanajiandaa kwa safari ya Stamford Bridge kukutana na Chelsea Jummaosi. City watakuwa wenyeji wa Huddersfield Jumapili.

JOE HART ATUA BRNLEY

BREAKING: Burnley Football Club imetangaza kumsajili Golikipa wa Manchester City Joe Hart kwa mkataba wa miaka miwili .

VILABU VYAHANGAIKA KUNASA SAHIHI ZA WACHEZAJI HUKU DIRISHA LIKIFUNGWA RASMI KESHO

Wakati muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili ukifika mwisho siku ya Alhamisi hii tutashuhudia vilabu vikinga'ng'ana kufikia mikataba ili kunasa sahihi za wachezaji mahiri kwa ajili ya msimu mpya 2018/2019
Klabu ya Liverpool ikionekana kufanya vizuri katika msimu wa usajili kwa kuongeza wachezaji wapya wanne huku akiweza kubakiza wachezaji wake mahiri wa msimu uliopita.
Manchester United inaonekana kutofanya vizuri mpaka sasa katika usajili hivyo kumfanya Kocha Jose kuwa mbogo huku akiona muda ukiyoyoma bila kuongeza mchezaji mpya katui ya wale aliowahitaji.
Je Tottenham hatimaye watamsaini mchezaji? Anthony Martial atabaki Manchester United?
Mlinzi  huyu mbelgiji Alderweireld alikumbwa na wakati mgumu kudumisha nafasi yake huko Tottenham baada ya jeraha kumweka nje msimu uliopita.Hivyo ameona ni vyema kutafuta timu yenye kumuhakikishia nafasi ya kucheza mechi msimu huu.
Mkataba wa Alderweireld unaisha mwisho wa msimu na kutokana na kuwa Manchester United wanammezea mate bei aliyowekewa ya pauni milioni 75 itakuwa kizuizi.Japo Kocha mreno Jose amepiga kelele kuwa CEO wa United haifanyii kazi listi ya wachezaji aliyompa.
Mshambuliaji huyu wa England amepitia misimu mitatu migumu huko Anfield kutokana na majeraha ya mguu wake hivyo kushindwa kucheza kwa misimu miwili na msimu uliopita kukabiliana na washambuliaji mahiri kama Mo Salah hivyo kukosa namba aliweza kucheza mechi nane na kafunga tu bao moja wakati wa mechi za Ligi ya Primia msimu uliopita.
Hilo hata hivyo halijawazuia the Reds kumwekea bei ya pauni milioni 20 mchezaji huyo huku ripoti zikisema kuwa Crystal Palace huenda wakamuhitaji.

TETESI USAJILI WA ULAYA KUELEKEA MWISHONI MWA MSIMU


Liverpool wanajiaanda kutuma ofa ya pili kwa  Monaco  kumsajili kiungo mchezeshaji mwenye umri wa miaka 22 Mfaransa  Thomas Lemar,baada ya mchezaji huyo kukataa kandarasi mpya ya kuitumikia Klabu yake ya  Ligue 1 . (Chanzo:Independent)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atarudi tena kwa Mualgeria Riyad Mahrez mwenye umri wa miaka 26 anayekipiga Leicester City's  mwishoni mwa msimu . (Mirror)

Luis Enrique, Kocha wa zamani wa Barcelona ambaye amehusishwa na kumrithi  Antonio Conte wa Chelsea, anajiandaa kuelekea Uingereza. Kocha huyo mwenye miaka  47 anataka kuchukua mikoba hiyo lakini iwe mpaka mwisho wa Msimu . (Telegraph)
Tottenham wanataka kumsajili Mfaransa  Abdoulaye Doucoure mwenye Umri umri wa miaka 25 anayekipiga  Watford . (Mail)
Mbrazil amabye ni beki  Fabinho, 24, ambaye  Manchester United walikuwa wakimnyatia msimu uliopita,amesema muda wake kuwa  Monaco ukaribia mwisho "coming to an end". (Metro)
Klabu ya Chinese Super League  Hebei China Fortune wanatayarisha ofa nyingine kwenda   Barcelona kuweza kumpata Lionel Messi, 30, baada ya ofa ya kwanza kukataliwa . (Mundo Deportivo - in Spanish)
Nottingham Forest wanataka kumsajili kipa mgiriki   Stefanos Kapino mwenye miaka 23 aliondoka  Olympiakos - ilipokuwa ikimilikiwa na mmiliki wa sasa Forest Tajiri  Angelos Marinakis baada ya kutokuelewana. (Sun)
Mshambuliaji  Benik Afobe, 24, yupo mbioni kurudi Wolves moja kwa moja kama vinara hao wa Championship wataweza kuingia EPL. Aliondoka  Molineux  kujiunga Bournemouth Januari 2016 lakini alirudi kwa mkopo  Januari. (Mirror)
Na Chediel Charles
Kwa msaada wa mitandao

WATFORD YAIKUNG'UTA CHELSEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI GOLI 4-1

*Mashabiki wamtupia lawama kocha Antonio Conte.
Watford walifunga magoli matatu dakika za mwisho ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Javi Gracia katika uwanja wa nyumbani katika usiku ambao hautasahaulika  na kuzidi kuongeza presha kwa Kocha Antonio Conte  wa Chelsea.
Timu hiyo inayofahamika kwa jina la 'The Blues' walicheza karibu saa nzima wakiwa pungufu watu 10  baada ya Tiemoue Bakayoko kupewa kadi nyekundu baada ya kucheza madhambi dakika ya 30 ya mchezo iliyopelekea Watford kupata nafasi nne.

Watford ambao wameshinda mara katika michezo 12 iliyopita  waliongoza baaada ya kupata penati kwa Gerard Deulofeu kujiangusha kirahisi wakati akikabiliana na Kipa Thibaut Courtois' na Troy Deeney kufunga penati hiyo..

Katika dakika ya 84 Daryl Janmaat alifunga goli la pili zuri  baada ya kutoka winga ya kulia kucheza 'one-two' Roberto Pereyra na kuwapita walinzi kadhaa wa Chelsea na kufunga kwakutumia mguu wake wa kushoto. 
Deulofeu aliongeza goli lingine katika dakika ya 88 baada ya kukimbia na mpira kutoka katikati ya Uwanja na kupiga shuti lililombabatiza  Gary Cahill  kabla ya   Pereyra kufunga goli la nne.

Magoli ya Watford yalifungwa na Deeney dakika ya 42,Janmaat 84,Deulofeu 88 na Pereyra 90
Wakati lile la Chelsea lilifungwa na Hazard 82 

Watford wapo na pointi sita zaidi kutoka kwenye timu zilizo kwenye hatari ya kushuka daraja.
Gracia, aliyechukua mikoba Marco Silva mwezi uliopita , aliviambia vyombo vya habari kuwa  "Ni ushindi mkubwa sana na mechi muhimu sana.Ninaona fahari kwa wachezaji wangu siku ya leo.

"Tumecheza mchezo mzuri,tuliwashambulia.Na mechi ilibadilika baada ya kutolewa nje Bakayoko,nafikiri tulicheza vizuri. Chelsea  ni timu kubwa na klabu kubwa."
Ni mcheoz wa pili mfululizo kwa kufungwa Chelsea baada ya kipigo 3-0 nyumbani na Bournemouth.
Na Chediel Charles
Kwa Msaada wa Mitandao.

LIVERPOLL WAMNYAPIA NYAPIA JACK WILSHERE IWAPO ATAKATAA MKATABA MPYA ARSENAL

ARSENAL wamempa ofa  kiungo huyo Muingereza lakini wameweka masharti mpaya ikiwemo kupunguza kiasi katika mshahara wake wa  pauni £90,000 kwa wiki.
Wilshere, mwenye Miaka 26, amekwama kwenye mazungumzo na Arsenal. lakini rekodi yake mbaya ya kuumia mara kwa mara inaonyesha mkataba wake mpya utategemea sana  na pafomansi yake uwanjani. 
Lakini  Jurgen Klopp yupo tayari  kumpa Wilshere mkataba wake wa sasa mwishoni mwa msimu akiwa mchezaji huru.
Klopp tayari ameshamchukua mchezaji mwingine wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain kwenye dili la pauni  £35 milioni.
Na inajulikana kwamba amekuwa akimuhusudu Wilshere ambaye anapambana kurudi kwenye timu ya Taifa ya Uingereza ili ashiriki World Cup.

Mjerumani huyo anamuhitaji kiungo huyo ili kuweza kuziba pengo  Emre Can ambaye anaonekana kuvutiwa na Juventus.
Can hajakubali kusaini kandarasi mpya Anfield  na Klopp amesema: “Wakati mwingine mchezaji anapenda kuona mkataba wake unafika mwisho, hili sio jambo zuri kwa Klabu ,lakini kipindi inabidi uikubali hali hiyo"


Gwiji wa Liverpool  Phil Thompson anaona  Wilshere  utakuwa ni usajili mzuri sana kwa wekundu hao.
Alisema: “Ningemchukua kuja Liverpool — ana uwezo mkubwa .”
“Nimekuwa nikimhusudu kwa muda mrefu.”
Maoni yake yaliungwa Mkono na mchezaji wa zamani wa Arsenal staa Paul Merson ambaye alisema: “Nadhani Liverpool watamchukua sio muda mrefu.”

THE 10 MOST EXPENSIVE DEALS OF THE JANUARY TRANSFER WINDOW


Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top