Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea tena usiku wa jana huku Man City akiwa ugenini mwa Basle pale ilipoitandika wenyeji hao kwa magoli 4-0 yakiwa yamewekwa kimiani na Sergio Kun Aguero alifunga moja ya bao ,na sasa Aguero anakuwa mchezaji wa pili kufunga katika michezo minne ugenini katika Champions League kwa timu zinazotokea Uingereza baada ya Dwight Yorke.
Lakini pia assist ya Kelvin De Bruyne katika bao la kwanza la Ikay Gundogan inamfanya Mbelgiji huyo kufikisha jumla ya assist 19 katika mashindano yote ikiwa ni assists 5 kuliko mchezaji yeyote EPL.
Kwa sasa kikosi hicho cha Pep Gurdiola wanakuwa wameshinda mechi nyingi hadi sasa (34) ikiwa ni idadi kubwa ya ushindi kuliko waliopata msimu mzima uliopita (33).
Juventus jana waliuanza kwa makeke mchezo wao dhidi ya spurs ambapo hadi dakika 10 za mwanzo walifanikiwa kufunga mabao 2 ndani ya dakika 10 za mwanzo kupitia Gonzalo Higuain ambaye baadae alikosa penati dakika ya 45+2
Tottenham walitokea nyuma kwa mabao mawili na kusawazisha kupitia Harry Kane dakika ya 35 na Christian Eriksen dakika ya 72 na sasa Harry Kane anakuwa mchezaji anayeongoza kwa mabao katika ligi kubwa 5 barani Ulaya (ana mabao 33).
Post a Comment