Coutinho ameaanza mara moja Barca toka ajiunge kutoka LIverpool Januari
Na Chediel Charles
Philippe Coutinho ametupia goli lake la kwanza Barcelona pale walipopambana na kuwafunga Valencia katika mchezo wa Copa del Rey.
Coutinho, amecheza mchezo wake wa watano toka alipojiunga kwa rekodi ya uhamisho wa £142m kutoka Liverpool, ni katika kipindi cha pili pale alipopewa majalo moja safi na Luis Suarez.
Hivyo kuwafanya Barca, mabingwa kwa miaka mitatu mfululizo kuongeza goli lingine kutoka kwa Ivan Rakitic dakika ya 82.
Barca watapepetana Sevilla katika mchezo wa fainali.
Valencia ambao wanashika nafasi ya 3 La Liga,wako na pungufu ya pointi 18 kutoka kwa vinara Barca.
Wakati matokeo yakiwa 0-0, striker Rodrigo alipiga mpira kichwa uliogonga mtambaa wa panya wakati Jasper Cillessen alionyesha umahiri wake kwa kuokoa mkwaju mkali kutkoa kwa beki wa kulia Jose Luis Gaya karibu kabisa baada ya Coutinho kufunga goli la kwanza.
Baada ya Rakitic kufunga kwa umahiri kutokana na kaunta ataki akimalizia pia pasi yaa Suarez, Barca walimuingiza Mkolombia mwenye umri wa miaka 23 beki Yerry Mina - aliyenunuliwa Januari kwa kiasi cha £10.4m.
Sevilla, waliopo nafasi ya sita wakiwa na pungufu ya pointi 25 kutoka vinara Barca,waliingia Fainali ya pili ya Copa del Rey ndani ya misimu mitatu kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya timu iliyopo La Liga , Leganes.
Barca wameshinda kombe hilo mara tatu mfululizo toka wapoteze kwa Real Madrid fainali ya 2014
.
Post a Comment