Kocha mwenye makeke mengi Jose Mourinho ameelezwa na mabosi wa Manchester United kubadili mbinu zake za usajili baada ya kuwa na msimu mbaya katika dirisha la usajili
Mashetani hao wekundu waliweza kunasa sahihi za wachezaji watatu tu na Mourinho amekasirishwa kwa Ofisa Mkuu Ed Woodward kushindwa kumuongezea wachezaji wengine.
Linatabainisha Gazeti la The Mirror , Mourinho ameambiwa na mabosi wake pale Old Trafford kubadilisha sera yake ya usajili kwa kutupia macho zaidi wachezaji wenye umri mdogo na wenye vipaji wanaoweza kudumu zaidi.
Ripoti zinadai maofisa wa United wamemuonya Mourinho kuacha kununua wachezaji wenye umri mkubwa na wenye gharama ambao wanakaribia kustaafu soka badala yake ajikite katika kuvumbua vipaji
Mourinho baada ya kuingia Old Trafford aliweza kumnunua Zlatan Ibrahimovic, Alexis Sanchez na Nemanja Matic na wengine ambao umri wao ni miaka 28 au zaidi walipokuwa wanajiunga na klabu hiyo kwa kandarasi nono .
Woodward aliamua msimu huu kutoruhusu kuondoka kwa Paul Pogba na Anthony Martial, japokuwa Mourinho alitamani waondoke.
Wafaransa hao ambao ni hazina ya muda mrefu katika klabu hiyo kutokana na kuwa umri mdogo hivyo kuona watawafaa kwa kucheza muda mrefu .
Bodi ya wakurugenzi ya United imeamua kuanzia sasa sera za usajili kuangalia zaidi wachezaji wenye manufaa ya muda mrefu ili kuendana na kasi ya Manchester City, ambao wamenunua wachezaji wenye umri na wenye vipaji na kuwaendeleza kama afanyavyo Pep Guardiola.
Post a Comment