Loading...
Home » Posts filed under Manchester United
MABOSI MAN U WAMPA MASHARTI MAPYA JOSE MOURINHO KUACHANA NA SERA YA KUNUNUA WACHEZAJI WAZEE
Kocha mwenye makeke mengi Jose Mourinho ameelezwa na mabosi wa Manchester United kubadili mbinu zake za usajili baada ya kuwa na msimu mbaya katika dirisha la usajili
Mashetani hao wekundu waliweza kunasa sahihi za wachezaji watatu tu na Mourinho amekasirishwa kwa Ofisa Mkuu Ed Woodward kushindwa kumuongezea wachezaji wengine.
Linatabainisha Gazeti la The Mirror , Mourinho ameambiwa na mabosi wake pale Old Trafford kubadilisha sera yake ya usajili kwa kutupia macho zaidi wachezaji wenye umri mdogo na wenye vipaji wanaoweza kudumu zaidi.
Ripoti zinadai maofisa wa United wamemuonya Mourinho kuacha kununua wachezaji wenye umri mkubwa na wenye gharama ambao wanakaribia kustaafu soka badala yake ajikite katika kuvumbua vipaji
Mourinho baada ya kuingia Old Trafford aliweza kumnunua Zlatan Ibrahimovic, Alexis Sanchez na Nemanja Matic na wengine ambao umri wao ni miaka 28 au zaidi walipokuwa wanajiunga na klabu hiyo kwa kandarasi nono .
Woodward aliamua msimu huu kutoruhusu kuondoka kwa Paul Pogba na Anthony Martial, japokuwa Mourinho alitamani waondoke.
Wafaransa hao ambao ni hazina ya muda mrefu katika klabu hiyo kutokana na kuwa umri mdogo hivyo kuona watawafaa kwa kucheza muda mrefu .
Bodi ya wakurugenzi ya United imeamua kuanzia sasa sera za usajili kuangalia zaidi wachezaji wenye manufaa ya muda mrefu ili kuendana na kasi ya Manchester City, ambao wamenunua wachezaji wenye umri na wenye vipaji na kuwaendeleza kama afanyavyo Pep Guardiola.
Filed Under:
Manchester United
on Friday, August 10, 2018
MOURINHO AWATOLEA MACHO WACHEZAJI 5 KABLA YA KESHO.
Mourinho anataka wachezaji wawili kabla ya kesho ambapo dirisha la usajili litafungwa rasmi Jerome Boateng, Harry Maguire, Toby Alderweireld, Sergej Milinkovic-Savic na Ousmane Dembele
Filed Under:
Manchester United
on Tuesday, August 7, 2018
JOSE MOURINHO:TUSIPOSAJILI WACHEZAJI WENGINE WAWILI AU WATATU TUTAKUWA NA MSIMU MBOVU SANA
Manchester United itakabiliwa na 'wakati mgumu' iwapo haitaongeza mchezaji yeyote katika dirisha la usajili linalokaribia kufungwa Alhamisi Kocha Jose Mourinho.
Mashetani wekundu hao wamemaliza msimu wa maandalizi kwa kipigo cha goli 1-0 dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich jana Jumapili.
Javi Martinez alifunga kwa kichwa cha kuparaza kipindi cha pili na kuwapa ushindi huo Bayern mechi iliyotawaliwa na mabingwa hao.
"Bosi wangu anajua ninachohitaji na imebaki siku chache ,nitasubiri na kuona kama tutaongeza mchezaji ," Mourinho alikiambia kituo cha MUTV.
"Vilabu vingine tunaoshindana nao wanatimu nzuri na imara sana. au wameimarisha kikosi vizuri sana kama Liverpool, ambao wamenunua kila kitu na kila mchezaji.
"Tusipoimarisha timu yetu vizuri huu utakuwa msimu mbaya sana kwetu."
United wameshasajili wachezaji watatu mpaka sasa - Kiungo MBrazil Fred kwa £47m, Mlinzi wa Kireno Diogo Dalot na golikipa chaguo la tatu Lee Grant.
Manchester United wanataraji kufungua pazia la EPL na Leicester City Uwanja Old Trafford siku ya Ijumaa.
Filed Under:
Manchester United
on Monday, August 6, 2018
Chediel . Powered by Blogger.