Wakati muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili ukifika mwisho siku ya Alhamisi hii tutashuhudia vilabu vikinga'ng'ana kufikia mikataba ili kunasa sahihi za wachezaji mahiri kwa ajili ya msimu mpya 2018/2019
Klabu ya Liverpool ikionekana kufanya vizuri katika msimu wa usajili kwa kuongeza wachezaji wapya wanne huku akiweza kubakiza wachezaji wake mahiri wa msimu uliopita.
Manchester United inaonekana kutofanya vizuri mpaka sasa katika usajili hivyo kumfanya Kocha Jose kuwa mbogo huku akiona muda ukiyoyoma bila kuongeza mchezaji mpya katui ya wale aliowahitaji.
Je Tottenham hatimaye watamsaini mchezaji? Anthony Martial atabaki Manchester United?
Mlinzi huyu mbelgiji Alderweireld alikumbwa na wakati mgumu kudumisha nafasi yake huko Tottenham baada ya jeraha kumweka nje msimu uliopita.Hivyo ameona ni vyema kutafuta timu yenye kumuhakikishia nafasi ya kucheza mechi msimu huu.
Mkataba wa Alderweireld unaisha mwisho wa msimu na kutokana na kuwa Manchester United wanammezea mate bei aliyowekewa ya pauni milioni 75 itakuwa kizuizi.Japo Kocha mreno Jose amepiga kelele kuwa CEO wa United haifanyii kazi listi ya wachezaji aliyompa.
Mshambuliaji huyu wa England amepitia misimu mitatu migumu huko Anfield kutokana na majeraha ya mguu wake hivyo kushindwa kucheza kwa misimu miwili na msimu uliopita kukabiliana na washambuliaji mahiri kama Mo Salah hivyo kukosa namba aliweza kucheza mechi nane na kafunga tu bao moja wakati wa mechi za Ligi ya Primia msimu uliopita.
Hilo hata hivyo halijawazuia the Reds kumwekea bei ya pauni milioni 20 mchezaji huyo huku ripoti zikisema kuwa Crystal Palace huenda wakamuhitaji.
Post a Comment