Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAGENI MASHUHURI WAZIDI KUVUTIWA NA MBUGA ZA WANYAMA TANZANIA.

Wikendi iliyopita nilipata fursa ya kumuaga mgeni mashuhuri mmojawapo aliyetembelea hifadhi zetu mwaka huu, baada ya Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Uswizi, Alain Berset na wachezaji soka wengi mara baada ya kombe la dunia tu kuisha. Huyu anaitwa Jack Nicklaus. Ni jina kubwa kwenye mchezo wa golf duniani. Unaweza kusema ni ‘Pele’ wa mchezo huu. Jina la umashuhuri wake wanamuita ‘the Golden Bear’.

Inasemwa ni mtu pekee aliyesanifu Viwanja vingi zaidi vya golf duniani kuliko mtu yeyote yule. Na sisi kwenye Wizara yetu tunakusudia kutumia mchezo huu kuvutia mikutano, mashindano ya kimataifa ya golf na utalii kwa ujumla huko mbeleni kupitia mchezo huu. Mbali na kwamba tumefaidika kwa ujio wake yeye na wanaye watatu na mkwewe mmoja, bali pia tumemhamasisha aje awekeze kwenye nchi yetu kwenye eneo hili, tukiamini uwepo wa mradi wake huo utatusaidia kupata watalii wengi zaidi na wa caliber hiyo. 

Ameahidi kuja tena kwa minajili hiyo. Lengo letu ni kuanzisha ukanda wa utalii ambao utakuwa karibu na ‘nature’ ili mtalii akija apate ‘experience’ ya kipekee, aweze kupata experience ya wildlife, sea/lake/beach, na ama mlima na msitu jirani na uwanja wa golf na hoteli yake, experience ambayo hawezi kuipata popote pale duniani! Kwa niaba ya Wizara, nilimkabidhi zawadi ya kinyago cha kimakonde. Pichani nikimuelezea ‘story’ inayoelezwa na kinyago hicho cha ‘ujamaa’. 

Wageni mashuhuri kama hawa wanapotembelea hifadhi zetu na wakiwa tayari kutupa muda wa mazungumzo tumeamua kuweka mkakati wa kuwatumia kutoa ‘endorsement’ yao ya destination Tanzania kwa maandishi na kwa video, na tutazitumia kwa matangazo, na pia tunawaomba wakawe mabalozi wazuri wa nchi yetu. 

Bahati mbaya sana hutokea, mara nyingi, baadhi ya watu mashuhuri, kama Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, wakakataa kutupa fursa hiyo, lakini tunaendelea kujaribu kufanya kila namna tupate endorsement yao kwa sababu tunaamini itatusaidia sana kwenye mikakati yetu ya kukuza idadi ya watalii kama washabiki wao wakiona kuwa hata hawa wameamua kwenda kupumzika Tanzania!


CHANZO: UKURASA WA CITIZENS FOR KIGWANGALA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top