Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Nape Nnauye:Tujisahihishe !!



Haya hatukukuzwa nayo.,wala si taratibu katika mila zetu kama watanzania. Katika utawala wowote lazima ziwepo changamoto ambazo serikali inalazimika kuzishughulikia, miongoni mwake ni migomo katika waajiriwa wa serikali, taasisi binafs na hata makundi ya watu yasiyo rasmi. Lakini kila mgomo una athari zake na namna ya kuumaliza.

Jamii ya watanzania imekuzwa katika Utaifa na Uzalendo. Kwa maana Taifa ni msingi wa mapambano ya mtu binafsi kisha yanafuata masuala binafsi. Huu ndio msingi tulioachiwa na waasisi wa Taifa hili. Kuachwa na kudharauliwa kwa misingi hii kunabadilisha namna ya maisha yetu, hatuhurumiani tena, hatusaidiani na wala hatupendani.

Wanalolifanya madaktari lina sura hii ya kubadilika kwa namna ya maisha yetu kwa sasa. Ni kweli maslahi ya kila mmoja wetu ni muhimu hasa katika kazi aliyoitolea jasho. Na hata nyongeza na mazingira mazuri ya kazi ni kitu cha msingi katika utendaji wa yeyote katika sisi,lakini sidhani kuwa kudai nyongeza kwetu na mazingira bora kunalazima kuacha fulani afe ukimtazama akiwa anakufa kwa kuwa si ndugu yako, wala si mtu unayemfahamu kwa ukaribu ama rafiki kwa kuona maslahi yako ni bora kuliko maisha ya mwingine, na bahati mbaya mwingine huyo hana uhusika wa namna yeyote katika kuzuilia ama kutozuilia maslahi hayo, hili si la kuungwa mkono kwa namna yeyote. TUNAPOTOKA kama jamii itaunga mkono hili na lazima wawepo watu miongoni mwetu wakukosoa ili TUJISAHIHISHE....!

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top