Wanamgambo wa kundi la Taliban waliojihami na silaha wamevamia hoteli mmoja mjini Kabul na kuzua mapambano makali na vikosi vya usalama nchini Afghanistan.
Maafisa wa usalama wanasema wanamgambo hao waliokuwa wamejihami na maguruneti na bunduki za rashasha walivamia hoteli ya Spozhmai ilioko kando kando ya ziwa Qargha.
Yamkini watu wawili wamefariki na wengine wakiwemo wanawake na watoto wametekwa nyara kufuatia tukio hilo.
Hata hivyo maafisa wa serikali wanasema watu 18 wameachiwa huru tayari.
Baadhi ya wageni wamelazimika kuruka kupitia kwenye madirisha ya hoteli kujisalimisha.
Taarifa zinadai kuwa kundi hilo limevamia hoteli hiyo kufuatia madai kuwa inatumiwa na mabwenyenye kuandaa sherehe ambazo zimeharamishwa na dini ya Kiislamu.
Matukio ya ghasia yameongezeka nchini Afghanistan katika siku za hivi karibuni.
Jumla ya wanajeshi watatu wa marekani na raia 20 wa Afghanistan wameuawa katika kipindi cha wiki moja iliopita.
Kwa Habari zaidi Tembelea BBC Swahili
Post a Comment