Mabingwa watetezi wa Kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya MAS Fes kutoka Morocco ilimaliza mechi bila wachezaji wake wanne na kuondolewa katika kinyanganyiro hicho na Athletic Club Leopards ya Congo Brazzaville 2-0 mjini Brazaville.
Klabu ya MAS iliyoiondoa Club Africain ya Tunisia kwa matuta mwaka jana kuwa klabu ya tatu kutoka Morocco kushinda Kombe hilo, ilimpoteza mcheza kiungo Rachid Dahmani aliyeonyeshwa kadi nyekundu kabla ya Bienvenu Kombo kufunga bao la Wacongo la kwanza mnamo dakika ya 40.
Refa kutoka Anngola alilazimika kuwafurusha mabeki wawili Omar Ennamsaoui na Said Hammouni katika dakika tano za mwisho kabla ya beki mwingine Younes Lyousfi naye kuona nyekundu katika dakika za majeruhi.
Licha ya upungufu huo klabu ya MAS iliweza kudhibiti hali ya mambo hadi Yapo Guolelida kufunga mkwaju wa peneti na kuiwezesha klabu yake kuingia hatua ya robo fainali.
Klabu hii Leopards kutoka mji wa Dolisie ulio magharibi mwa nchi iliweza kuvuka kipigo cha duru ya kwanza kwa kuinyuka klabu ya Tunisia CSS 2-0 nyumbani kwao Sfax.
Wacongo hao pia waliiondoa klabu nyingine kutoka Jamhuri ya Afrika ya kati Tempete Mocaf na Heartland ya Nigeria kwenye michuano mingine ya kufuzu kuingia hatua ya makundi, ambapo washiriki watajishindia kitita cha dola za Marekani 165,000 zawadi.
Klabu nyingine Black Leopards ya Afrika ya kusini nayo iliwashangaza wengi bila kutarajiwa kwa kuingia duru ya tatu ingawa ililazimishwa suluhu 0-0 dhidi ya Al Merreikh ya Sudan, washindi wa mwaka 2007 licha ya kunyukwa 3-2 mjini Omdurman majuma mawili kabla.
Watani wa Mereikh katika Ligi ya nyumbani Al Hilal pia walipiga hatua kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Cercle Bamako nchini Mali kupitia bao la kipindi cha kwanza lililofungwa na Mudathir Eltaib baada ya mabao mawili ya mchuano wa kwanza.
Vilabu vingine vya Mali navyo vilinusurika ambapo Stade Malien ililazimisha sare ya 1-1 na COD Meknes ya Morocco nyumbani kwao na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya bao 4-1.
Djoliba nayo ilipenya kupitia matuta baada ya kupoteza mchuano wa kwanza 2-0 nyumbani kwa Club Africain mjini Tunis. Abdelali Essamlali aliipa klabu yake Meknes matumaini kwa bao mnamo dakika ya 21, lakini Lamine Diawara akarudisha kabla ya mapumziko. Hamzi Agrebi aliongezea matumaini ya Africain kwa bao la pili lakini Haj Massaoud kurudisha kupitia mkwaju wa peneti ikiwa zimesalia dakika saba. Hatimaye ilibidi mchuano uamuliwe kwa matuta ambapo Djoliba ilishinda kwa 4-3.
Klabu pekee ya Morocco iliyonusurika na Wydad Casablanca, iliyotoa suluhu dhidi ya AFAD Djekanou ya Ivory Coast na kupiga hatua kutokana na ushindi wa ugenini.
chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment