
Milio ya bunduki imesikika leo katika kambi ya jeshi karibu na
uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
Waziri wa ulinzi wa Madagascar aliliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP,
kwamba kulitokea uasi jeshini, lakini haijulikani wanajeshi hao wanataka
nini.
Waziri huyo wa Ulinzi Jenerali Lucien Rakotoarimasy hakusema wanajeshi
wangapi walihusika.
Milio ya risasi imesita, lakini safari za ndege zimezuwiliwa.
Madagascar imekuwa ikipita kwenye misukosuko tangu mwaka wa 2009, wakati Marc
Ravalomanana alipopinduliwa na jeshi.
Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment