
Waliahidi kumpokea kwa mbwembwe na jana walikamilisha ahadi yao mashabiki wa klabu hiyo walijitokeza kwa wingi kumpokea Uwanja wa Kimataifa wa ndege jijini Dar es Salaam lakini kubwa kuliko lote ni kuvalishwa kwa jezi yenye jina la RAGE mchezaji huyo mara tu baada ya kupokelewa.
Vilabu hivi viwili ambavyo ni watani wa jadi wamekuwa mabingwa wa mbwembwe za magazetini ambazo tunashindwa ziona ndani ya Uwanja mara waingiapo kwenye mashindano ya kimataifa wao ni Mabingwa pande hizi za fitna Soka kama hivyo wameshampiga bao mtani wao na tena kumvalisha jezi yenye jina la Mwenyekiti wao hadharani kwanini usiwaite mabingwa kwa hilo Lakini ndani ya Uwanja mbona hatuoni umahiri wa timu hizii.Tunawasikia TP Mazembe,Zamalek na wengine timu zetu maneno yamekuwa mengi no na Wanachama wa timu hizonao wanalea haya ambayo kwayo wanaona ni ya manufaa zaidi kuliko umahiri wa timu Uwanjani hali hii mpaka lini ?
Post a Comment