Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akimkaribisha Mstahiki Meya wa manispaa hiyo Jerry Slaa kuzindua Jarida la ‘Sauti ya Ilala’ ambapo amesema kwa kuwa Ilala ndio lango kuu la kuingiza na kutoa bidhaa nchini kupitia bandari, pia ipo Ikulu, viwanda vikubwa na hoteli kubwa za kisasa, jarida hilo linayo mengi ya kuwaambia wananchi wake na watanzania kwa ujumla juu ya maliasili, fursa na nini kinaendelea na kutokea ndani ya manispaa.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (katikati) akizungumza wakati alipozindua jarida la ‘SAUTI YA ILALA’ ambapo amesema kwa sasa halmashauri hiyo inajiendesha kisasa sana, wanakusudia kuwa na jarida ambalo kweli litafanya kazi ya kuitangaza Ilala, na kufikisha ujumbe si tu kwa wananchi wa Ilala bali kwa Jamii nzima.
Aidha amewataka wafanyabiashara wa Ilala kujitangaza katika gazeti hilo ili fedha zitakazopatikana sio tu zitalipia gharama za uchapishaji bali fedha zitakazobakia zitatumika kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii. Kulia ni  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Paul Wanga na Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu, Mkurugenzi wa Kampuni 361 Mustafa Hassanali, Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Kheri Kessy.
Wageni waalikwa wakipitia toleo la zamani la Jarida la Sauti ya Ilala kabla ya uzinduzi rasmi.
Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa tatu kulia) na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Kheri Kessy wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa ‘Jarida la Sauti ya Ilala’.  Wanaoshuhudia tukio hilo Kulia ni Mh.Sada Madwangwa, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Paul Wango na kushoto ni Mkurugenzi  wa Kampuni ya 361 Mustafa Hassanali ambao ndio waandaaji wa uzinduzi huo.
Sasa limezinduliwa rasmi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (katikati), Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Kheri Kessy (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa wakikata keki yenye mfano wa jarida hilo  kwa pamoja mwendelezo wa uzinduzi wa Jarida hilo.
Wageni waalikwa wakisoma jarida hilo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakipitia jarida hilo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia) akipata picha ya ukumbusho na Mmoja wa wadhamini wa jarida la Sauti ya Ilala Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd. Bw. Imran Karmali (katikati).
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimshukuru mmoja wa wadhamini wa Jarida hilo Meneja Masoko na Afisa Uhusiano wa Benki ya Exim Linda Chiza.
..........................................................
Manispaa ya Ilala kwa kuelewa umuhimu wa habari na haki ya wananchi wake kupashwa habari na kujua mustakabali mzima Manispaa yao imerejesha na kuzindua upya jarida lake linaloitwa ‘SAUTI YA ILALA’.
Jarida hilo limebuniwa upya na kuongezwa vionjo vipya vya fani na maudhui vitakavyo mvutia msomaji ikiwemo habari za manispaa, habari za biashara ndani ya manispaa nakadhalika.
Akizindua jarida la ‘SAUTI YA ILALA’ katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es Salaam, Meya wa Manispaa ya Ilala Mstahiki Jerry Silaa amesema dhima yake ni kuhakikisha kuwa Ilala inakuwa kitovu cha uchumi wan chi na kufanya maeneo ya katikati ya mji kuwa sehemu safi, nzuri na inayovutia.
Ameongeza kuwa kwa kupitia jarida hilo watu wataweza kuona shughuli mbali mbali za kiuchumi zinazofanyika na pia kuona mafanikio yake.
Naye Afisa Uhusiano wa manispaa ya Ilala Bi. Tabu shibu akizungumzia Jarida hilo amesema ‘SAUTI YA ILALA’ mpya inakwenda kugusa wengi kwa sababu jarida limebuniwa upya kuweza kukidhi matakwa ya watu wa rika, uchumi, elimu na Nyanja mbambali hivyo wananchi watakaopata fursa ya kulisoma  watafurahia ladha tofauti.

Chanzo na MO BLOG