Polisi nchini Kenya, wanasema kuwa watu zaidi ya 50 waliuawa siku ya Jumanne usiku wa kuamkia Jumatano, kufuatia mapigano makali kati ya jamii za Pokomo na Orma katika eneo la Mto Tana Kusini Mashariki mwa Kenya.
Mauaji hayo yilitokea wakati watu wenye silaha kutoka jamii ya Pokomo waliposhambulia kijiji kimoja katika eneo la Reketa huku wakiteketeza makaazi ya watu.
Pia kutokana na mauaji hayo sasa watu wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na kuwa wanahofia kushambuliwa.
Jamii ya Pokomo ni wakulima na huwa inategemea sana mto wa Tana kwa shughuli zao.
Jamii ya Orma ni wafugaji.
Mapigano hayo ambayo yametokea wakati nchi hiyo ikiwa na kumbukumbu za vurugu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007 zilizosababisha watu zaidi ya 1,200 kufariki kutokana na vurugu hizo wakati wa cuhaguzi.
Post a Comment