Msukuma mkokoteni akisukuma mkokoteni uliojaa kuni kwa ajili ya
kuchomea matofali kama alivyonaswa na kamera yetu mjini Mpanda katika
eneo la Kawajense namba mbili, uchomaji matofali kwa kutumia kuni
kunachangia sana katika uharibifu wa mazingira na uangamizaji wa
misitu ya asili na kusababisha ukame katika mkoa wa Katavi ndiyo maana
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda juzi alitoa wito kwa wana Katavi kuacha
kabisa kukata miti kwa lengo la kuchoma matofali na badala yake
watumie pumba za mpunga kwa shughuli hizo.
Post a Comment