Jenerali Ulimwengu akitoa Mhadhara katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika kituo cha Kinondoni ambapo leo ilikuwa ni siku ya Kitivo cha Sayansi ya Jamii,ambapo alizungumzia namna maadili yalivyoporomoka nchini Tanzania.
Mkuu wa Kitivo,Dk.Ngaruko(Wa pili kutoka kulia) ,Prof.Mbwiliza(wa kwanza kushot) wakimsikiliza kwa makini Jenerali Ulimwengu aliekuwa akitoa Mhadhara leo tarehe 8/9/2012 katika Ukumbi wa Kituo cha Kinondoni,Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Washiriki wakifuatiliana kwa makini mhadhara huo kutoka kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Elimu Endelevu Dk.Kisoza akiwa na Dk.W.A.Pallangyo
DK.Mary D.N.Kitula akichangia mada baada ya mtoa mhadhara Jenerali Ulimwengu kumaliza kuongea
Mwanafunzi wa mwaka pili katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii ambae jina lake halikufahamika mara moja akichangia katika Mhadhara
Wengi wa washiriki walikuwa ni wanafunzi ambao walijumuika na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania waliweza kusikiliza kwa makini Mhadhara ikiwa ni sehemu ya wao kujifunza na kuweza kupata maarifa mapya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 20 Dk.Kihwelo pia alikuwa ni mmojawapo ya waliobahatika kuchangia katika mhadhara huo ulioongelea kinachosababisha kumomonyoka kwa maadili katika jamii yetu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Mr.Maulana akiwa ni mmojawapo ya wajumbe wa kamati inayosimamia Maadhimisho ya Miaka 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania akisikiliza kwa makini mhadhara uliozungumzia kiini/kisababishi cha kuporomoka kwa maadili katika jamii.
Hii ikiwa ni Muendelezo wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Jenerali Ulimwengu ni mmoja wapo ya wageni walioalikwa kuja kutoa Mhadhara asubuhi ya leo.Kuanzia Saa Nane tunatazamia kuwa na Ugeni wa Waziri MKuu Mstaafu Mhe.Frederick Tluway Sumaye
Post a Comment