Waziri mmoja wa Kenya amekanusha kuwa amehusika na wizi wa gari moja la rais ambalo amekutwa nalo.
Waziri wa Serikali za Mitaa, Fred Gumo,
alisema gari lake alikuwa amempa mfanya biashara alioko Mombasa na
badala yake akakabidhiwa hilo gari, ambalo lilikuwa limeibiwa kutoka kwa
rais wa zamani, Daniel Arap Moi, miaka mine iliyopita.
Bwana Gumo alisema hakujua kuwa gari hilo lilikuwa la kuibiwa.
Alisema hakulitumia sana kwa sababu hakupata nyaraka zote za gari hilo.
Chanzo:BBC Swahili.
Post a Comment