Wizara
ya Maliasili na Utalii imefafanua kuwa barabara ambayo nchi ya
Ujerumani imependekeza kuwa ingependa kuifadhili ni ile ambayo inaanzia
Mto wa Mbu mkoani Arusha kwenda Mkoani Mara kwa kupitia nje ya Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti upande wa Kusini. Barabara iliyopendekezwa
haitapita kabisa ndani ya Hifadhi hiyo.
Ufafanuzi
huu umetolewa baada ya magazeti mawili ya hapa nchini yanayotolewa kwa
lugha ya Kiingereza (toleo la tarehe 4 Septemba) kuandika kuhusiana na
barabara hiyo bila kuweka wazi kuhusu ramani ya barabara ambayo Naibu
Balozi wa Ujerumani aliitaja hivi karibuni alipomtembelea Waziri wa
Maliasili na Utalii
Aidha,
gazeti mojawapo kati ya hayo mawili, toleo la tarehe 5 Septemba 2012
liliandika tahariri iliyoonyesha kuwa barabara iliyopendekezwa itapita
ndani ya Hifadhi ya Serengeti upande wa Kaskazini, hiyo siyo kweli maana
Naibu Balozi hakusema hivyo.
Mazungumzo
kuhusu suala hili la barabara ya Serengeti yalifanyika tarehe tarehe 3
Agosti 2012 wakati Naibu Balozi wa Ujerumani wa hapa nchini Bw. Hans
Koeppel alipomtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Khamis
Kagasheki na kumwambia kuwa nchi yake iko tayari kufadhili upembuzi
yakinifu na ujenzi wa barabara itakayozunguka Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti upande wa Kusini kama nchi hiyo itaombwa kufanya hivyo. Waziri
Kagasheki alilipokea pendekezo hilo na kuahidi kulipeleka kwa Waziri wa
Ujenzi Mhe Dkt Magufuli.
George Matiko
MSEMAJI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Tarehe 8 Septemba 2012
Simu: +255 784 468047
Loading...
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment