Kwa habari kutoka TFF kuwa mashabiki 61 walishuhudia mechi kati African Lyon na Polisi Moro na ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na Polisi Moro iliyofanyika Septemba 19 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Ni habari ya kutustua kidogo haswa ukizingatia ni juzi tu kwenye mechi ya ufunguzi African Lyon waliletewa mizengwe walipopata mdhamini mpya.
Lakini baada ya mechi hii waliyopata watazamaji 61 tu unajiuliza busara ipo wapi hapa kuizuia Klabu hii kuwa na mdhamini mwingine ambae atasaidia timu hii iweze jitosheleza na pia kuisadia kuweza kujenga timu nzuri ya ushindani ili Kiwangoi cha soka Letu kiweze kukua.
Na haya ndio Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 5,000 ni sh. 185,000. Baadae Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 20,287.91 pesa hii sizani hata nauli kwa timu inatosha na ni utani mwingine huu pale unapokataa timu isiwe na mdhamini wa ziada mbona hukomajuu tunakoambiwa tuwe kama wao wana wadhamini wengi tena zaidi ya wawili wanaotoa huduma sawa iweje kwetu hapa na mapato haya ?
Pia mgawo mwingine ni huu asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 27,457.62 na tiketi sh. 89,916.Hawa ndio walipata sehemu kubwa ya kasungura hako walipogawana.
Kuna wengine nao walioambulia japo Kasungura hako nao ni Kamati ya Ligi sh. 6,762.63, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,057.58, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,703.05, gharama za mchezo sh. 6,762.63 na uwanja sh. 6,762.63.Napo kuna maswali hapa inakuwaje hawa nao wanapata kamgawo ka kasungura hako ilhali hatuoni jitihada zozote wanazofanya ili soka liweze kusonga mbele.
Je kwa mahudhurio haya kuna busara yeyote kuwazuia African Lyon na vilabu vingine viweze kupata mdhamini ambae anaweza kuzisaidia timu hizi ? Busara iko wapi hapa !
Ligi Kuu Tanzania Bara inachangamoto nyingi sana zinazotakiwa kutatuliwa na vilabu vyetu vinaendeshwa kimaskini sana na mfano ni juzi kocha wa Yanga alipolalamika kuwa alishindwa hata kuoga alipotoka Mbeya kwani Hotel waliyofikia haikuwa na maji hawa ni Yanga je timu nyingine ndogo kilio chao kitakuwaje?
Busara inahitajika hapa na tunakaribisha kwa mikono miwili kukutna kwa Klabu zote na Wadhamini Vodacom huenda neema itapatikana kupitia Kikao hicho kwa afya njema ya Soka letu la Tanzania.
Post a Comment