Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WALIOTEULIWA TUME YA POLISI WAONGEZA MATUMAINI YA UCHAGUZI WA AMANI NCHINI KENYA

Ofisa wa polisi wa Kenya akilinda doria mitaa ya Mombasa. Baada ya wajumbe wa Tume ya Taifa ya Jeshi la Polisi kuthibitishwa, polisi watakuwa chini ya mamlaka moja. [Simon Maina/AFP]

Kaimu Katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kimemia aliwatangaza waliyoteuliwa tarehe 6 Septemba na majina yaliwasilishwa kwa bunge siku iliyofuata. Bunge limepewa hadi tarehe 28 Septemba kupitia waliyoteuliwa na kuomba majina mapya kama kutakuwa na wowote watakaokataliwa.
Mchakato wa kuanzisha NPSC ulikuwa umecheleweshwa tangu Agosti 2011 kwa sababu ya kutokubaliana kati ya Waziri Mkuu Raila Odinga na Rais Mwai Kibaki kuhusu waliyoteuliwa.
Waliyopendekezwa katika tume ni Johnstone Kavuludi kama mwenyekiti, na Ronald Musengi, Esther Chui-Colombini, Murshid Mohamed, Major Muiu Mutia na Mary Owuor kama wajumbe.
NPSC itakuwa na madaraka ya kuchunguza, kuajiri, kufukuza, kuadhibu na kuwahamisha maofisa wa polisi. Tume pia itasaidia kutekeleza masharti mapya ya katiba ya kuweka chini ya makao makuu uongozi wa vitengo mbalimbali vya polisi, ambavyo awali vilifanya kazi kwa kujitegemea.
"Kuundwa kwa tume ni hatua kubwa ambayo itasaidia kurekebisha jeshi letu la polisi na kutoa muundo muhimu wa kupambana na hali ya kutokuwa na usalama na kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki," alisema Fred Kapondi, mwenyekiti wa kamati ya idara ya bunge ya Utawala na Usalama wa Taifa.

Kupambana na ugaidi na vitisho kwa uchaguzi wa amani

Chama cha Sheria cha Kenya (LSK), ambacho kilikuwa kinashinikiza marekebisho ya polisi, kimeyapokea mabadiliko, kikisema tume itaimarisha shughuli za polisi.
"Ni mwelekeo chanya ambao utasaidia kuongeza amani na kutoa msukumo zaidi katika operesheni inayoendelea ya kulinda mipaka ya Kenya kuhusiana na vita dhidi ya al-Shabaab," Mwenyekiti wa LSK Erick Mutua aliiambia Sabahi. "Makamishna wapya ni wataalamu wenye taarifa za rekodi nzuri na tunaamini kwa pamoja wataweka damu mpya ambayo inatakiwa ili kulifanya jeshi la polisi la Kenya kufanya kazi zaidi na kushughulikia uhalifu."
LSK imeelezea ucheleweshaji katika uteuzi wa inspekta jenerali wa polisi na wasaidizi wake wawili kama tatizo kuu.
Mara tu itakapoundwa, NPSC itateua wasaidizi wawili wa inspekta jenerali wa polisi na mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID), baadaye jopo maalumu litamteua inspekta jenerali.
Kabla ya kutekelezwa kwa katiba mpya mwaka wa 2010, Kamati ya kupitia Katiba ya Kenya (CKRC) iliwahoji wadau na kugundua kwamba mfumo wa sera uliyovunjika ulikuwa unaongoza katika kutoelewana ambako kulileta kutojali kwa usalama.
Wajumbe wa vyama vya kiraia waliwaambia CKRC kwamba kuwaweka polisi chini ya amri ya NPSC kutawafikisha katika oparesheni ya mtazamo mzuri dhidi ya magaidi na vitisho vya uchaguzi wa amani.

Kuimarishwa kwa jeshi la polisi katika ugawaji wa madaraka

Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ya mwaka 2010, serikali imekuwa ikipitia mchakato wa kugatua madaraka ya taasisi za serikali kwa awamu; mchakato ambao ulipangwa kukamilika na kuanza kufanya kazi baada ya uchaguzi wa mwezi Machi 2013.
Kugawa madaraka ya taasisi za serikali inahusisha uhamishaji wa baadhi ya madaraka katika serikali za nchi na utengaji wa wakala za serikali nchi nzima katika jitihada za kurahisisha upatikanaji.
Chini ya mpango unaopaswa, NPSC itawajibika kwa jeshi la polisi linalohusika na shughuli zake katika kitengo kipya kinachopaswa, ambacho kinatarajiwa kusaidia mfumo wa kueneza usalama karibu na watu.
NPSC pia inatarajiwa kuandaa taratibu za kinidhamu za haki na wazi kulingana na Ibara ya 47 katika katiba na kuchunguza na kuitwa kwa ajili ya ushahidi wakati wa uchunguzi.
Kuanzishwa kwa NPSC "sio tu ni ishara kwamba demokrasia ya Kenya imekomaa, lakini pia ni kiashirio kipya kwa wawekezaji wa nje kuona kwamba wanasiasa wa Kenya sasa wamekomaa vya kutosha kukaa na kukubaliana kwa pamoja kuhusu masuala muhimu ya utawala", alisema James Shikwati, mkurugenzi wa kituo cha wataalamu wa kiuchumi, Mtandao wa Kiuchumi Katika Kanda.
Kuundwa kwa NPSC imekuwa kipaumbele baada ya vurugu zilizofuatia uchaguzi wa mwaka 2007, katika jitihada za kuhakikisha kwamba mashirika ya usalama wa nchi yatabaki huru katika migogoro ya kisiasa kwa siku zijazo.
Shikwati aliiambia Sabahi kwamba uteuzi wa NPSC utasaidia pia kuondoa wasiwasi miongoni mwa wawekezaji kuhusu usalama wa uwekezaji wao.
"Wawekezaji wengi wana wasiwasi kwa sababu wengi walipoteza mali wakati wa vurugu zilizoibuka baada ya mabishano ya uchaguzi wa mwaka 2007," alisema. "Wanataka kusimamisha uwekezaji wao hadi baada ya uchaguzi, lakini wakati taasisi ya kuaminika kama NPSC inapowekwa na kufanya kazi, inawapa ujasiri wa kubaki na kuendelea kuwekeza zaidi."
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top