Makamu Mkuu wa Chuo,Prof.Tolly Mbwete akiongoza kwa vitendo pale alipo waongoza wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kufanya usafi eneo la chuo na linalokizunguka chuo pembezoni mwa Barabara ya Kawawa leo asubuhi.
Kaimu Makamu MKuu wa Chuo(RS),Prof.Varisanga nae alikuwa bega kwa bega katika shughuli ya kuyafanya usafi ambapo wafanyakazi wote walijitokeza kufyeka,kusafisha mitaro na kufagia ili kuyaweka safi maeneo yanayozunguka chuo leo asubuhi Kinondoni pembezoni mwa barabara ya Kawawa.
Kaimu Makamu MKuu wa Chuo(RS),Prof.Varisanga nae alikuwa bega kwa bega katika shughuli ya kuyafanya usafi ambapo wafanyakazi wote walijitokeza kufyeka,kusafisha mitaro na kufagia ili kuyaweka safi,hapo akitoa uchafu kutoka kwenye mtaro pembezoni mwa barabara ya Kawawa.
Dk.Kihwelo akiwajibika ndani ya mtaro kuondoa makaratasi yanayoziba mitaro hiyo na kufanya maji machafu kutuama na kusababisha mazalia ya mbu.
Kazi ilikuwa ni moja kuzibua pale ambapo hapakuwa sawa,mdau akiwajibika vilivyo
Kazi na dawa ! Wakiwa wanafanya kazi huku wakipiga stori mbili tatu ili kuweza kuongeza nguvu na kazi isonge ni Sia Machenje(alijifunga kanga) na Ombeni(mwenye shati la drafti) wakipiga soga kidogo.
Prisca Kasalama na Ingrid Dyauli wakiwajibika vilivyo katika kuyaweka katika hali ya usafi maeno yanayokizunguka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Makao Makuu ya Muda ,Kinondoni leo asubuhi.
Cheko sasa !!
Mdau nae hakuwa nyuma
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina adhimisha miaka 20 toka kianzishwe Mwaka 1992 mwishoni mwa mwezi Oktoba,2012,leo wafanyakazi walijumuika na uongozi wa Chuo kufanya usafi kwa kusafisha mitaro,kufyeka nyasi na kufagia ili kuyaweka safi.
Post a Comment