Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama(Mwenye suti ya Kijivu) akipata maelezo ya utafiri wa miche bora ya kahawa kutoka kwa wataalamu wa Tacri
Mmoja kati ya wafanyakazi wanaosaidiana na wataalamu wa Tacri katika kuzalisha miche bora ya Kahawa
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama akishuhudia baadhi ya miche iliyozalishwa na Tacri ikiwa tayari kwa ajili kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima kwa ajili ya kuoteshwa
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Leonidas Gama(Katikati) na mkuu wa wilaya ya Hai,Mhe Novatus Makunga(kulia) akipata maelezo kuhusiana na msitu wa asili unaotunza na Tacri kutoka kwa mtaalamu wa taasisi hiyo
Na Mwandishi Wetu,Hai
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mhe Leonidas Gama ametangaza mkakati maalumu wa kufufua zao la kahawa katika mkoa huo kwa kuitumia ipasavyo Taasisi ya utafiti wa Kahawa Nchini(TACRI) ambayo ipo wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo katika ziara yake wilayani Hai ambapo katika ziara hiyo ya siku tatu alipata fursa ya kutembelea taasisi hiyo na kujionea shughuli mbalimbali za utafiti wa zao la Kahawa.
Mhe. Gama ameeleza kuwa halmashauri zote saba za wilaya katika mkoa wa Kilimanjaro zitalazimika kuandaa mkakati wa kukitumia kituo hicho katika kufufua zao la kahawa ambalo kilimo chake kimeporomoka sana mkoani humo.
“Ukizungumzia Kilimanjaro ni kahawa na ukizungumzia kahawa ni Kilimanjaro hivyo ni vyema sasa tukaja na mkakati kabambe wa kufufua zao hilo kwa ajili ya kuinua uchumi wa wananchi wetu,mkoa na taifa kwa ujumla,”alisisitiza
Mhe. Gama ameeleza kuwa tayari wilaya kama ya Mbinga mkoani Ruvuma imeweza kuinua zao la Kahawa kutokana na halmashauri ya wilaya hiyo kukitumia vyema kituo cha utafiti wa kahawa kilichoko wilayani humo.
Chanzo:Hai Blog
Post a Comment