Hapa akijibu swali.Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama akiongea na waandishi wa habari ofisini
kwake kuhusiana na tukio la kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Liberetus Ballow usiku wa Kuamakia leo maeneo ya Kitangiri.
Nyumba
ya Dorcas Moses mwalimu wa shule ya Msingi ya Nyamagana ambye alikuwa
kwenye gari aina ya Rav 4 aliyepewa lifti na kamanda Ballow usiku
kumrudisha kwake. Hapa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Fredrick
Katulanda akitoka kufanya mahojiano.
Mtoto
wa kaka yake Mwalimu Dorcas akiongea kuhusiana na tukio la Kifo cha
kamanda Ballow ambapo yeye ndie alikwenda kufungua geti kwa ajili ya
Mama yake Dorcas aweze kuingia ndani ila kabla ya kufungua ndipo
aliposikia risasi ikipigwa.
Hapa ni nyumbani kwa marehemu kamanda Ballow.
Hili
ndilo geti ambalo kifo cha kamanda Ballow kilipotokea usiku wa kuamkia
leo wakati mwalimu Dorcas Mosese alipokuwa akirudi nyumbani kwa lifti ya
gari la Kamanda Ballow.
Baadhi ya jamaa yake marehemu nyumbani kama walivyokutwa na kamera yetu.
Jamaa zake marehemu Ballow.
Waombolezaji wa kike wakilia kwa uchungu nyumbani kwa kamand Ballow leo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Ballow ameuwa usiku wa kuamkia
leo na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu
na Hotel ya Tai Five majira ya kati ya saa saba hadi nane.
Haya
yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni
Mkuu wa Mkoa Mwanza Injinia Everest Ndikillo wakati akitoa taarifa za
tukio la kuuawa kwa Kamanda Ballow.
Tukio
hilo ambalo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa jiji la Mwanza pamoja
na familia yake huku watu wa kijiuliza kuhusiana aliyehusika na mauuaji
hayo ya kikatili.
Taarifa
ya Mkuu wa Mkoa zinasema kuwa Kamanda Ballow alikiuwa anatoka katika
kikao cha harusi na ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa
kinafanyika katika Hotel y a Florida na kish akumpelek amwanamke aitwaye
Dorcas Moses Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Nyamagana maeneo ya barabara
ya Kona ya Bwiru kwenda Kitangiri.
Walipofika
getini kwa Mama Dorcas mara waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa makoti
ya PolisiJamii, Mama Dorcas alimuuliza Kamanda Ballow kama anawafahamu
Kamanda akasema kuwa hawa na watu wa ulinzi wa Jamii wako doria.
Mara
wale watu waliongezeka na kuwa sita wakaanza kama kuzozana wao kwa wao
na ndipo Kamanda alipowauuliza kuna nini, Mmoja wao akajibu hakuna kitu
na ikapelekea Kamanda kutaka kutoka nje ila wale watu watatu
wakaizingira gari ya Kamanda Ballow aina ya Rav 4.
Kamanda
Ballow alipoona kama hali hewa inabadilika alichukua redio call ili
aweze kuwa taarifu askari na ndipo wale jamaa walipompiga risasi
kichwani nakupelekea kifo chake.
Taratibu
za mazishi ya Kijeshi bado zinaendelea na nyumbani kwa marehemu ambapo
mwandishi wa blogu hii amefika na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika
hali ya majonzi sana. Mke wa Kamanda Ballow yuko Dar es Salaam na
anatarajia kufika Mwanza.
Mpaka sasa Polisi wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Dorcas kwa ajili ya Mahojiano huku uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na kifo cha kamanda Liberetus Ballow.
Via Mwanza yetu
Post a Comment