Muigizaji ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Ramadhani Mkiety maarufu kwa jina la Sharo Milionea, amekufa.
Kijana huyo maarufu, aliaga dunia jana jioni baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka, akafa papo hapo.
Alipata ajali katika kijiji cha
Lusanga, Muheza akiwa katika gari lenye namba za usajili T478 BVR
Toyota Harrier, jana jioni.
Mwili wa marehemu Sharo Milionea upo katika Hospitali Teule ya Muheza.
Chanzo:Maisha Blog.
Post a Comment