Bwana Zuma, ambaye ana wake zaidi ya mmoja na watoto 21, anasifika sana kama mwenye kufuata itikadi za utamaduni wa Zulu.
........................
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewataka wazee wa jadi au wahenga kumsaidia katika kushikilia uongozi wa chama tawala (ANC).
Bwana Zuma alihudhuria sherehe moja kijijini
siku ya Jumapili, ambako ng'ombe 12 walichinjwa na huku ubani ukichomwa
watu wakimuombea achaguliwe tena.
Wapinzani wake wanataka ang'olewe kutoka katika uongozi wa chama, huku kongamano la chama likitarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Bwana Zuma, ambaye ana wake zaidi ya mmoja na watoto 21, anasifika sana kama mwenye kufuata itikadi za utamaduni wa Zulu.
Alimshinda mtangulizi wake Thabo Mbeki katika kinyang'anyiro kikali kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka
2007 ili kuongoza chama cha ANC.
2007 ili kuongoza chama cha ANC.
Mkuki na Ngao
Ushindi wake ulimaanisha kuondoka mamlakani kwa
bwana Mbeki na kumweka Kgalema Motlanthe kama rais wa mpito, hadi mwaka
2009 ambapo uchaguzi mkuu ulifanyika na kumuingiza madarakani.
Tawi la vijana wa chama tawala pamoja na maafisa wengine wa serikali sasa wanamfanyia kampeini bwana Motlanthe, ambaye ni makamu wa rais, kumenyana na bwana Zuma katika kongamano litakalofanyika mwezi ujao, mjini Mangaung.
Wawili hao watakuwa wakigombania uongozi wa chama.Familia ya Zuma ilichinja ng'ombe 12 na kuchoma
ubani katika kijiji chao cha Nkandla mkoani KwaZulu-Natal siku ya
Jumapili kuwataka wahenga kumpa mwongozo kabla ya uchaguzi.
"tuko hapa kumtakia kila keri baba yetu. Baada
ya sherehe hii tuna imani kuwa ana ulinzi wa kutosha na tuna uhakika
atarejea kusherehekea nasi.'' alinukuliwa akisema mwanawe Zuma ,
Nomthandazo Zuma
Kiongozi wa kijamii alimpa Zuma mshale na ngao
akiwa amevalia nguo yenye madoa doa na kumtaka atumie silaha hiyo
kujikinga kutokana na wapinzani wake katika chama cha ANC.
Bwana Zuma amekumbwa na kashfa za ufisadi tangu
alipochukua mamlaka lakini kulingana na duru za kisiasa huenda
akachaguliwa tena.
Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment