Baadhi ya Wajumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. |
Bw. Julius Chisi, Naibu Mpimaji Ardhi Mkuu kutoka Malawi akizungumza machache wakati wa mkutano huo. |
Baadhi ya Wajumbe wengine kutoka Malawi akiwemo Mhe. Chiyaonga (kulia), Balozi wa Malawi hapa nchini. |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo. |
Mkutano kati ya Tanzania na Malawi kujadili suluhu ya mgogoro
wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa umeanza katika ngazi ya Wataalamu jijini Dar es
Salaam tarehe 15 Novemba, 2012.
Mkutano huo unaowahusisha
wataalam kutoka Wizara na Idara mbalimbali za Serikali za Tanzania na Malawi unafanyika Jijini Dar
es Salaam katika Hoteli ya Serena.
Akifungua Mkutano huo Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule alisisitiza
umuhimu wa wajumbe kutoka nchi zote mbili kujadili na kupendekeza njia
zitakazosaidia kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huo.
Aidha, Bw. Haule aliweka bayana kuwa
Serikali ya Tanzania ina
dhamira ya dhati kufanya kazi pamoja na Serikali ya Malawi kutafuta suluhu ya mgogoro
huo jambo ambalo pia lilisisitizwa na Bw. Julius Chisi, Kiongozi wa Ujumbe wa
Malawi.
Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku tatu
hadi tarehe 17 Novemba, 2012 umeanza na Kikao cha Wataalamu ambacho kitafuatiwa
na kikao cha Maafisa Waandamizi na kuhitimishwa na kikao cha Mawaziri tarehe 17
Novemba, 2012.
Chanzo; http://foreigntanzania.blogspot.com
Post a Comment