Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

AGIZO LA OCD ARUSHA LAANZA KUFANYIWA KAZI



Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Hatimaye wakazi wa Njiro Mtaa wa Kitalu “D” wameanza kutekeleza agizo la
Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto
lililowataka waanzishe kikundi cha ulinzi shirikishi katika eneo lao.

Jana mwandishi wa habari hizi aliwasiliana na Mwenyekiti wa eneo hilo Bw. John Kihwele kwa nia ya kujua utekelezaji wa mpango huo ambao ulitokana na kikao kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo kiongozi huyo alisema kwamba, wananchi wa eneo hilo kwa sasa wamekuwa na muamko mkubwa mara baada ya kuhamasishwa na Mkuu huyo wa Polisi wa Wilaya kupitia mkutano wa Ulinzi shirikishi uliofanyika mwezi uliopita katika eneo hilo.

“Kwanza kabisa ndugu Mwandishi namshukuru sana OCD maana wananchi wangu wamekuwa na morali ya hali ya juu sana mara baada ya mkutano ule maana mpaka hivi sasa ninapoongea na wewe tayari tumeshaingia mkataba na kampuni moja ya ulinzi iitwayo FODEY SECURITY ambayo itakuwa inafanya doria usiku kwa kutumia gari katika mtaa wetu”. Alifafanua Bw. Kihwele ambaye ni Mwenyekiti wa eneo hilo.

Alipoulizwa kwa nini wameamua kutumia kampuni ya ulinzi badala ya askari
wao, Mwenyekiti huyo alisema wameamua kufanya hivyo ili ulinzi wao uwe wa
kisasa zaidi na kuongeza kwamba suala la gharama si tatizo kwani wananchi
wameielewa vizuri elimu ya ulinzi shirikishi iliyotolewa na jeshi la polisi hivi
karibuni ndio maana kwa pamoja na kwa moyo mkunjufu wameamua kutekeleza agizo hilo.

Katikati ya mwezi Novemba mwaka huu Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto alifanya mkutano na wakazi wa eneo hilo kwa nia ya kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi. Katika mkutano huo Mwenyekiti alitoa lawama zake kwa wananchi wake kwamba baadhi yao hawataki kuchangia vikundi hivyo kwa madai kwamba wanajitosheleza katika suala la ulinzi kwa kuwa wameajiri makampuni na walinzi binafsi.

Mara baada ya Mkuu huyo wa Polisi wilaya ya Arusha kupata taarifa hiyo aliwaelimisha kwa kuwapa faida ya vikundi vya ulinzi shirikishi na kisha kuwaambia kwamba suala hilo si la hiyari bali ni lazima na yeyote ambaye hatatoa mchango serikali ya Mtaa inaweza kumchukulia hatua kupitia sheria ndogo ndogo za serikali hiyo ambayo itatungwa na wao wenyewe baada ya kukubaliana.

Kupitia Mkutano huo Mkuu huyo wa Polisi wilaya ya Arusha aliamua kuonyesha
juhudi kwa vitendo kuhusiana na uanzishaji wa kikundi cha ulinzi shirikishi eneo hilo, mara baada ya kufanya harambee ya kushtukiza kwa wakazi hao huku yeye akiwa wa kwanza kutoa fedha mfukoni mwake na hatimaye kupatikana Tsh 125,000 taslimu papo hapo.

Toka kuhamishiwa wilaya ya Arusha kwa Mrakibu huyo Mwandamizi wa Polisi
ambaye alikuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi ya Kawe Mkoa wa Kipolisi
wa Kinondoni Kanda maalum ya Dar es salaam amekuwa akifanya mikutano ya
mara kwa mara katika maeneo mbalimbali na kutoa elimu juu ya Polisi Jamii na kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi.

Mpaka hivi sasa baadhi ya maeneo ambayo tayari amekwishafanya mikutano
na wananchi, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na viongozi wa kata na mtaa ni Sokoni One, Njiro kitalu “D”, Sekei na katika bwalo la Maofisa wa Polisi ambapo alikutana na wenyeviti karibu wote wa Halmashauri ya jiji la Arusha.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top