Sir Alex Ferguson, meneja wa Manchester United,
Jumamosi alielezea kwamba hajawahi kuona ulinzi mbovu wa timu yake msimu
huu kama alivoshuhudia wakati timu yake ikiwa ugenini Reading, licha ya
kuondoka na ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya wenyeji.
Robson akifunga goli kwa kicwa kunako dakika ya 8 ya mchezo na kuwafanya reading kuongoza kwa goli 1.Picha na Daily Mail.
United mara nyingi walionekana dhaifu kutokana
na mchezo wa kupanga na kuviziana, na meneja Ferguson alisema ni lazima
timu yake kuinua kiwango cha mchezo wao kufikia mwishoni mwa wiki ijayo,
wakati watakutana na majirani Manchester City.
Anderson akipiga mkwaju ulienda moja kwa moja wavuni likiwa ni goli la kusawazisha kwa Manchester United.Picha na Daily Mail.
"Ulikuwa ni ulinzi mbovu zaidi msimu huu," alielezea Ferguson.
“Lazima tuchukue hatua kuhusu hili”.
Rooney akitumbukiza kwenye kamba mkwaju wa Penati na kuifanya Manchester United Kuongoza kwa 2 kwa 1 la Reading.Picha na Daily Mail.
"Reading waliweza kuelekeza mipira vyema, lakini kabisa mlikuwa hamna ushindani katika kuzuia hayo."
Adam Le Fondre katikati akiisawazishia Reading kwa kufunga goli la pili,hivyo mchezo kurudi tena kuwa mgumu kwa pande zote mbili.Picha na Daily Mail.
Mara mbili walilemewa na kuwaacha Reading
kutangulia kwa magoli, na hii ikiwa ni mara ya 14 msimu huu kuiacha timu
ya upinzani kutangulia kupata bao la kwanza.
Magoli yote saba ya timu zote mbili yalifungwa katika dakika 34 za kipindi cha kwanza katika uwanja huo wa Madejski.
Reading walichukua usukani kwa muda pale Morrison alipoifungia timu hiyo goli la 3 kwa 2 ya Manchester United na kuwaweka katika wakti mgumu Man U.Picha na Daily Mail.
Rooney akitumia pasi murua toka kwa Evra akiirudisha mchezoni timu yake kwa kuisawazishia goli la 3 hivyo ngoma kuwa Reading 3 na 3 Manchester United.Picha na Daily MAil.
Kwa bahati nzuri, Man U waliweza kujibu
mashambulizi ya Reading mara mbili, na kuongezea magoli ambayo
yaliwawezesha kurudi Old Trafford na ushindi, na wakiwa kileleni mwa
ligi ya Premier, sasa tofauti kati yao na wapinzani wao wakuu, majirani
Man City, ni pointi tatu.
Van Persie akaifungia timu yake shuti lililoamua mshindi wa mechi hiyo kwa kuifungia Manchester UNited goli la 4 hivyo kuondoka na pointi tatu muhimu.Picha na Daily Mail.
Man City, wakiwa nyumbani katika uwanja wao wa Etihad, watawakaribisha Man United Jumapili ijayo.
"Tulistahili kutandikwa leo," alisema Ferguson.
"Hakuna aliyefanya juhudi za kushindania
migongeo. Pasipo kupendelea, Reading walimiliki mpira vyema, kijana
[Nicky] Shorey aliwaelekezea wenzake mipira vyema mno. Tulistahili
kufanya vyema zaidi ya hivyo. Tulicheza vibaya mno”, alilalama Ferguson.
"Iwapo utafanya makosa kama hayo katika ulinzi,
basi kila wiki kazi yako itakuwa ni juhudi za kuokoa tu. Leo ilikuwa ni
juhudi zaidi za kuokoa tu.
"Ilikuwa ni muujiza namna tulivyoshinda kwa ulinzi kama huo. Ninaridhika tu kwa kuwa tuliondoka na ushindi.”
"Ilikuwa ni muujiza namna tulivyoshinda kwa ulinzi kama huo. Ninaridhika tu kwa kuwa tuliondoka na ushindi.”
Chanzo cha Habari;www.bbc.co.uk/swahili
Picha na daily Mail
Post a Comment