Mafundi wakivunja Nyumba iliyokuwa katikati ya Barabara baada ya mmiliki wa nyumba hiyo kukubali fidia ya 260,000 yuan ($41,000) nyumba hiyo ilikuwa imebaki yenyewe katikati ya barabara ya Wenling huko katika Jimbo la Zhejiang na kubomolewa Dec. 1, 2012.
Pichani ni nyumba hiyo ambayo wameliki wake walikataa kuivunja wakipinga kupewa malipo kiduchu ya fidia hivyo nyumba hiyo kubaki peke yake na katikati ya Barabara.
Kutoka katika Kijiji cha Xiayangzhang chifu Chen Xuecai alisema kwamba nyumba hiyo imevunjwa Jumamosi baada ya mmiliki wake mkulima Luo Baogen na mke wake, kukubali kupokea fidia ya yuan 260,000($41,000).
Luo, mwenye 67, alikuwa ndio ametoka kumaliza kujenga nyumba yake kwa gharama ya Yuan 600,000($95,000) wakati serikali ilipokuja na kumuambia kuwa watamlipa fidia ya Yuan 220,000 ($35,000) kuondoka kwenye nyumba hiyo na Bwana Luo akagoma malipo hayo akidai ni madogo kulinganisha na gharama aliyotumia kuijenga nyumba hiyo.Baadae wakapandisha fidia hiyo hadi Yuan 260,000($41,000) wiki iliyopita na kukubalika baada ya kukutana na maafisa wa Serikali.
Chanzo:Nbc News


Post a Comment