Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUTOKA KWA LADY JAY DEE:GHARAMA NA UTARATIBU NITAKAOUTUMIA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Natoa Jambo sana kwenu nyote:
Nilipata maswali kwa watu ambao walionyesha nia ya kutaka kuambatana na mimi na crew yangu kwenda kuukwea Mlima mrefu Afrika, Kilimanjaro.

Na mimi bila hiana nimeona si vibaya nikiwafahamisha utaratibu wote, ili kwa atakaeweza kushiriki tuongozane nae pamoja
Tutaondoka Dar es salaam kuelekea Moshi tar 6 January 2013
Kwa njia ya anga... 
Kwa wanaotokea Dar au mikoa mingine watalazimika kujilipia nauli za Ndege au Bus au kama ni magari yao binafsi ni sawa pia, ila tar 6 January 2013 tunakutania Moshi, Kilimanjaro.
Tutalala hapo kwa usiku mmoja huku tukisubiri kuianza safari ya Mlimani siku inayofuata.
Gharama za safari ya kupanda mpk kileleni na kushuka ni US$ 500 (Dola za kimarekani mia tano) kwa mtu mmoja
Hiyo gharama ina cover Milo mitatu kwa siku, Wabeba mizigo, Guides, Chef, Camping gears na Hifadhi ya kulala tangia siku unapofika Moshi mpk siku utakayoondoka

Japo kuna vitu kadhaa utalazimika kununua kwa gharama tofauti na hiyo endapo utavihitaji.
Vitu kama Pombe, mavazi ya baridi ya kuongezea n.k

Tunaanza kupanda Mlima tar 7 January 2013 na tar 12 January 2013 tunakuwa tumekamilisha safari yetu hiyo, itakayotuchukua siku 5.

Kuhusu maswala ya afya kila mtu anafahamu afya yake ni muhimu mkajiangalie kwa madaktari mpate ushauri kabla ya kuamua kwenda kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mimi binafsi niko fiti, ki afya na kimazoezi.

La msingi zaidi linaloshauriwa ni kutayarisha fikra zako tu ziwaze kupanda na kumaliza bila pupa, 
Ukianza uoga tu hufiki juu.
Oooh watu wanaugua, watu wanakufa wewe jiamini bwana.
Waliopanda wakafika wana nini mpaka si tushindwe?

Gate tutakaloondokea ni MARANGU GATE

Natumaini kwa maelezo hayo mtakuwa mmepata kufahamu vya kutosha na kuamua kama mnakuja na mimi au la??
Ukiwa tayari kwenda tuwasiliane ili ni comfirm idadi ya watu.

Deadline ni tar 1 January 2013.

Niandikie e-mail: judyjaydee@yahoo.com
Subject iwe: MT.KILIMANJARO ili nipate urahisi wa kuzifungua mail zinazohusiana na safari hiyo

Niwatakie heri ya mwaka mpya in advance.
Much Love to you all:
JIDE
 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top